17 July 2012
Vodacom yahitimisha Wajanja Tour
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imehitimisha msimu wa kwanza wa Tamasha la 'Wajanja Tour' mkoani Tanga.
Tamasha hilo lilizinduliwa Dar es Salaam, Morogoro, Mtwara na mwishoni mwa wiki limefanyika Tanga.
Akizungumza mjini hapa juzi na waandishi Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema tamasha hilo lilifanyika katika Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni katika kukamilisha msimu wa kwanza wa mfululizo wa matamasha yaliyofanyika kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.
“Tamasha hili la Mkoa wa Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani lilifanyika katika kukamilisha msimu huu wa kwanza. Tunajipanga kwa ajili ya msimu wa pili wa kutoa burudani kwa Watanzania.
"Tunawahakikishia wateja wetu kuwa tamasha hili halitaishia hapa, tunaangalia namna ya kwenda katika mikoa mingine kwani watu wengi wamevutiwa na burudani wanayoipata hivyo tunaangalia uwezekano wa kwenda mikoa mingine ya Tanzania Bara na Zanzibar,” alisema Nkurlu.
Alisema lengo la Tamasha la Wajanja Tour si tu kutoa burudani, pia ni njia pekee ya kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao na kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao zaidi,” alisema.
Nkurlu alisema Tamasha hilo la Wajanja wa Vodacom pia limekuwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujiunga na kupata huduma mbalimbali kutoka mtandao wa Vodacom Tanzania.
Alisema kampuni hiyo imeanzisha huduma zinazowawezesha kurahisisha matumizi ya simu kwa kuongea kwa robo shilingi, kutuma ujumbe kwa sh. 25 kwenda mtandao wowote hapa nchini na kuperuzi facebook na twitter bure.
"Pia wateja wa Vodacom wananufaika mno na huduma ya intanet hasa vijana ikiwemo ofa ya wajanja intaneti, inayompa mteja huduma ya intaneti kwa sh. 250 kwa siku, pamoja na ofa ya simu za Nokia Asha kwa sh. 75,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment