23 July 2012

Uwamsho Zanzibar walianzisha tena


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

JESHI la Polisi jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi wa Jumuiya ya Uwamsho ambao walikuwa wamekusanyika katika viwanja vya Mbuyuni kufanya ibada.

Kazi ya kuwatawanya wafuasi hao haikuwa rahisi ambapo baada ya kuondolewa, polisi waliimarisha doria katika viwanja hivyo na maeneo mengine jirani.


Wafuasi hao walikusanyika karibu na Msikiti wa Mbuyuni wakitaka kufanya Mhadhara wa mwisho bila kupata kibari cha polisi ili kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Awali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipiga marufuku mikusanyiko yote isiyo na kibali cha polisi ikiwemo mihadhara baada ya jumuiya hiyo kufanya vurugu zilizosababisha uvunjifu wa amani kuchoma makanisa pamoja na magari.

Katika vurugu za awali, Barabara za Michenzani ziliharibiwa vibaya baada ya wafuasi hao kuchoma matairi moto katikati ya barabara ambapo wafanyabiashara wa maduka katika maeneo ya Mbuyuni, Darajani na Mikunguni walilazimika kufunga maduka yao

No comments:

Post a Comment