20 July 2012

TSA yaomba kusaidiwa kwenda Kenya



Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha Kuogelea Tanzania (TSA), kimewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha safari ya waogeleaji 19 na viongozi wawili wanaotakiwa kwenda kushiriki mashindano ya Afrika yanayotarajia kufanyika Septemba 10 hadi 16 mwaka huu Nairobi, Kenya.


Mashindano hayo ya wazi yanatarajia kufanyika kwa siku 7 katika mabwawa ya kuogelea ya Moi Kasarani jijini humo, huku kila nchi ikiruhusiwa kusajili waogeleaji wawili kwa kila tukio, ambapo jumla ya nchi 10 zitashiriki.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Ufundi wa TSA, Marcelino Ngalioma alisema maashindano hayo ni makubwa na yanaweza kuwasaidia wachezaji kupata uzoefu zaidi, lakini pia kuiletea sifa nchi kwa kunyakua ubingwa.

"Tunaimani wachezaji wetu watafanya vizuri katika mshindano hayo, ambayo tunashiriki kama nchi mwalikwa hivyo tunaomba sapoti ya kila mdau kutuwezesha kuipeleka timu hii kushiriki mashindano hayo," alisema.

Alisema timu hiyo imegawanyika katika makundi mawili ya wanawke na wanaume ambapo ili kusafirisha timu hiyo, yenye jumla ya waogeleaji 19 wanahitaji kiasi cha sh. 44,520,000 zinahitajika ili kuwasafirisha pamoja na viongozi wawili.

"TSA wameona kunauwezo wa kupunguza gharama za usafiri na hivyo wameamua timu hiyo iondoke kwa usafiri wa basi, ambapo itaondoka nchini Septemba 8 mwaka huu kushiriki katika mashindano hayo.

Wachezaji waliochaguliwa kwa wanawake Magdalena Moshi, Mariam Foum, Ashna Tanna, Gouri Kotecha na Neena Patel.

Kwa upande wa wanaume ni Jamal Talib, Mophat Oswald, Issa Rashid, Nassor Salmini, Omari Abdallah, Michael Mathias, Adam David Kitururu, Hilal Hilal na Ammar Ghadiyali.

Wengine ni Hines Msingo, Aliasger Karimjee, Patrick Kimimba, Gourav Kotecha na Adil Bhurmal.

Alisema wachezaji hao wataandaliwa mashindano ya Taifa Septemba Mosi hadi 2, mwaka huu Dar es Salaam ili kujipima.

No comments:

Post a Comment