20 July 2012

TFF yatuma salamu za rambimbi ajali ya meli



Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya meli ya Mv Skagit iliyotokea juzi na kupoteza maisha ya abiria wengi waliokuwemo kwenye chombo hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema ajali hiyo mbaya iliyotokea karibu na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ni msiba mkubwa, si kwa wadau wa mpira wa miguu pekee, bali kwa wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"Hivyo tunatoa pole na salamu za rambirambi kwa ndugu wa marehemu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na wote walioathirika na kuguswa na msiba huo mkubwa," alisema Wambura.

Alisema kutokana na msiba huo, mechi mbili za jana za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) kati ya Atletico ya Burundi na El Salam Wau ya Sudan Kusini na ile ya Mafunzo ya Zanzibar, dhidi ya Tusker ya Kenya zilichezwa huku wachezaji wa timu zote wakiwa wamevaa vitambaa vyeusi.

Wambura alisema mbali ya vitambaa hivyo, pia kulikuwa na dakika moja ya kukaa kimya kwa ajili ya kuomboleza vifo hivyo, kabla ya kuanza mechi hizo zilizochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment