20 July 2012
Abdala Juma hatukuelewana vizuri
Na Victor Mkumbo
MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Simba, Abdallah Juma amesema timu yake haikucheza katika kiwango cha kuridhisha katika kipindi cha kwanza juzi dhidi ya Ports ya Djibouti kwa hawakuelewana.
Simba na Ports zilikutana juzi katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame ambapo mabingwa hao wa Tanzania Bara waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Akizungumza baada ya mchezo huo juzi uliopigwa Uwanja wa Taifa, Juma alisema katika kipindi cha kwanza hawakucheza katika kiwango kilichotakiwa.
Alisema wachezaji walionekana kuudharau mchezo kutokana na kuwa Ports, kuonekana kuwa ni moja ya timu vibonde katika michuano ya mwaka huu.
Mshambuliaji huyo alisema, Milovan Cirkovic aliona upungufu kipindi cha kwanza ndipo alipofanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji kipindi cha pili.
Alisema nguvu alizoongeza kocha kipindi cha pili, ndizo zilizoifanya timu hiyo ishinde kwa mabao 3-0 wakati yeye akiwa amefunga mabao mawili.
"Kipindi cha kwanza timu ilicheza bila kuelewana, lakini baada ya mabadiliko tulicheza mpira wa kushambulia na kupiga pasi ndefu ndiyo zilizotufanya tuibuke na ushindi," alisema.
Katika mechi hiyo Simba ilikosa mabao mengi, huku mshambuliaji wake Mzambia Felix Sunzu alikosa mabao zaidi ya nane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment