02 July 2012
Serikali yaombwa kununua vitanda vya wajasiriamali
Na Anneth Kagenda
WAJASILIAMALI nchini wanaotengeneza vitanda vya wanawake vya kujifungulia mahospitalini wameiomba Serikali kutoa vipaumbele kwa kununua bidhaa hizo ili kuwaongezea kipato kikubwa wazawa wa ndani.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana kwenye maonesho ya wajasiliamali Mkurugenzi wa Kampuni ya Senga Boys Workshop yenye Makao Makuu yake Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa wanaomba serikali itekeleze ombi lao ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono badala ya kuagiza vitanda hivyo nje wakati vinapatikana nchini. .
"Tumekuwa tukishuhudia serikali ikisema kuwa ina upungufu wa vitanda vya akina mama kuzalia labda haina taarifa kwamba kuna wazawa wake wanavitengeneza hivyo basi tunaomba ituunge mkono ili tuweze kupata ongezeko kubwa la kipato," alisema
Uagizwaji wa vifaa nje ya nchi ni moja ya sababu inayoweza kulipunguzia Taifa pato kutokana na kwamba kuna bidhaa nyingi zikiwemo za kichina zinatengenezwa lakini wakinunua hapa nchini wanakuwa na imani kwamba hatuwezi kutengeneza vitu feki," alisema.
Alisema kuwa vitanda hivyo ambavyo huuzwa kwa gharama nafuu tofauti na vile vya nje ya nchi vimekuwa vikitengenezwa kwa uimara wa hali ya juu huku vikiwa na vifaa mbalimbali vya kisasa ambavyo vinamuwezesha mama kujifungua vizuri na kupata mtoto bila tatizo lolote.
Bw. Senga alisema kuwa pamoja na utengenezaji wa vitanda hivyo vyenye ubora lakini wajasiliamali hao wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali na kubwa ikiwa ni ile ya upungufu wa vitendea kazi na masoko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment