06 July 2012

Redd's Miss High Learning kupatikana leo


Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya kumsaka mnyange wa Redd's Miss High Learning 2012 yanatarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Maisha uliopo Oysterbay, Dar es Salaam.

Warembo 14 wanatarajiwa kupanda jukwaani kuwania taji hilo, ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mashindano ya urembo kujua nani atafanikiwa kuondoka nalo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo, Agnes Mathew kinyang'anyiro hicho klinatarajiwa  kuanza saa 2 usiku, ambapo kutakuwa na burudani za kukata na shoka.

“Kila kitu kimekamilika, kwa sasa tunachosubiri ni kupata mshindi tu,” alisema Agnes.

Agnes alisema, burudani zinatarajiwa kutolewa na Bob Junior, Mashujaa musica na Peter Msechu.

Katika shindano hilo, mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 2, wa pili Sh milioni 1, wa tatu Sh 800,000, wan ne Sh 500,000, wa tano Sh 250,000 na waliobaki watapewa kifuata machozi cha Sh 150,000 kila mmoja.

Shindano la Redds Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment