03 July 2012

NHC yasaini mkataba bil. 165/-, ujenzi wa nyumba




Na Grace Ndossa

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), imetiliana saini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 165 na benki tisa nchini ili kufanikisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu ambazo zitakopeshwa kwa wananchi.

Hafla ya kutiliana saini iliyofanyika Dar es Salaam jana na kushuhudiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Benki zilizosaini mkataba huo ni CRDB, ECO, Benki ya Uwekezaji Tanzania, ABC, NMB, CBA, Azania na Taasisi ya Kifedha ya Shelter Afriqe. Shirika hilo pia limeingia mkataba na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (LAPF).

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu, alisema fedha hizo zitasaidia kuanza ujenzi wa nyumba za bei nafuu ambazo baadaye watakopeshwa wananchi wa kipato cha chini kuanzia sh. milioni 25 hadi 50.

Alisema mkopo huo umetokana na shirika hilo kupewa kibari na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kinachowawezesha kukopa katika taasisi za fedha zilizopo ndani na nje ya nchi.

“Kutokana na mkopo huu, miradi ya ujenzi imeanza kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini kama Dar es Salaam, Kigoma, Arusha, Dodoma na mingine ipo njiani kutekelezwa,” alisema.


Aliongezea kuwa, mwaka huu shirika hilo litajikita kwenye ujenzi wa miradi ya bei nafuu ambapo upembuzi yanikifu unaendelea nchi nzima ili kutambua Wilaya ambazo zitahusishwa na miradi hiyo.

“Mkopo huu tutaanza kuulipa baada ya miaka minne, nyumba za bei nafuu zitaanzia sh. milioni 25, 35, 50 hadi 200.

Kwa upande wake, Prof. Tibaijuka, alizipongeza benki hizo kwa kulipa shirika hilo mkopo ambao utatumika kujenga nyumba hizo.

Alisema shirika hilo limejidhamini lenyewe bila kuitegemea Serikali na wanapaswa kulipa deni hilo kwa wakati lakini Serikali itaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa katika maoneo ya wazi

No comments:

Post a Comment