23 July 2012

Mtanzania Rajabu kuzichapa na Mnamibia



Na Mwali Ibrahim

BONDIA wa Tanzania Rajabu Maoja wa Tanga anatarajia kupanda ulingoni na bondia Gottlieb Ndokosho wa Namibia katika pambano lao la ubingwa wa IBF litakalofanyika Septemba Mosi katika jiji la  Wlndhoek nchini humo.


Pambano hilo linatarajia kuwa katika uzito wa kg 75 raundi 12 lililopewa jina la 'The Battle of the Kalahari Desert' litasimamiwa na Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi ambaye pia ni Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Rais huyo ilisema pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kinda Boxing Promotion ya nchini humo chini ya promota Simon Nangolo ambalo linawakutanisha mabondia hao wenye historia kwa kila mahali walipotoka.

"Mpambano huu utakuwa mzuri sana na wakusisimua kwani ni mpambano pekee kwa bondia wa Tanzania kuwania nje ya nchi ubingwa huu wa Afrika ukiachilia ule wa mwaka 2000 uliokuwa kati ya Iraq Hudu na Ali Said uliofanyika, Mombasa, Kenya," alisema.

Aliongeza kuwa mabondia hao wanapanda ulingoni huku Rajabu akiwa tayari amecheza mapambano 31, aliyoshinda yakiwa ni 18, alipoteza 10 na Sare tatu huku Gottlieb yeye akiwa amecheza mapambano 15 alishinda ni 11, amepoteza tatu na sare 1.

No comments:

Post a Comment