23 July 2012
Shindalo la Miss Utalii Mwanza lafutwa
Na Mwali Ibrahim
BODI ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililofanyika hoteli ya New Mwanza hivi karibuni kufuatia taifa kuwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, iliyotokea mjini Zanzibar Jumatano iliyopita na kupoteza uhai wa watu wengi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari juzi jijini Dar es Salaam na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Miss Utalii Tanzania, Abubakari Omary Bakari, ilisema shindano hilo limefanyika kimakosa na matokeo yake hayawezi kutambuliwa kwa namna moja ama nyingine.
Alisema uamuzi wa serikali ni wa mwisho, hivyo hawajaunga mkono kufanyika kwa shindano hilo wakati nchi ina majonzi ya kupoteza ndugu na jamaa zao.
“Shindano limefanyika bila kuzingatia misingi ya kiubinadamu na uzalendo kwa Taifa, hivyo Bodi imeamua kulifuta na waandaaji watafuata tena utaratibu mwingine na kuliandaa upya," alisema.
Aliongeza kuwa “Miss Utalii ni shindano lenye uzalendo, hivyo inapotokea matatizo kama haya na agizo la maombolezo kutoka kwenye serikali nadhani kuna kila sababu ya kuliafiki,” ilisema taarifa hiyo.
Shindano hilo liliandaliwa na Fania Beauty Salon, chini ya Mkurugenzi wake Fania Hassan, ambaye sasa ana changamoto nyingine ya kujiweka sawa katika jamii, ukizingatia kwamba Taifa lilikuwa kwenye maombolezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment