23 July 2012

Majimaji yawalilia waliofariki kwa ajali ya Meli


Na Mhaiki Andrew, Songea

BODI ya uongozi  wa klabu ya Majimaji ya Songea umepokea kwa masikitiko na simazi kubwa juu ya vifo vya Watanzania wenzetu ambavyo zilisababishwa na ajali ya kuzama kwa meli ya MV. Scargeti, ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar na kusema Taifa limepoteza vijana ambao baadhi yao wangeweza kuibuka kisoka  na  kuwa nuru kwa nchi.

Akizungumza mjini hapa kwa niaba ya Bodi  hiyo. Mwenyekiti wa Wanalizombe hao, Humphrey Milanzi alisema  pamoja na Taifa kupoteza nguvu kazi wake katika ajali hiyo ya meli, bado Wanaruvuma kupitia klabu za soka wanaungana na Taifa katika kuombeleza msiba huo ambao umeleta simanzi na majonzi makubwa ambayo hayawezi kusaulika kamwe.

Alisema katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika maombolezo ya kuwaombea wenzetu waliokufa katika ajali hiyo  ya meli na wale wahanga wake walionusurika katika ajali hiyo , wamewataka Watanzania hasa wale ndugu zao waliopoteza maisha wawe watulivu wakati vyombo husika vikiendelea na uchunguzi wake  kuweza kubaini tatizo ambalo lilisababisha ajali hiyo.

Alisema Majimaji ambayo inajiandaa na mashindano ya ligi ya Taifa ya Daraja la kwanza kusaka kupanda Daraja na kucheza ligi kuu itakumbukwa muasisi wake, marehemu, Dkt Lawrence Mutazama Gama alikuwa kipenzi cha watu na alikubalika  kila kona ya nchi pale alipofikia hatua ya kutoa  wazo la kuundwa kwa timu  hususani soka na kufanikiwa.

Timu ya Majimaji kwa sasa imeanza mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo ya kusaka kupanda Daraja na kucheza ligi kuu, huku ikiendelea na mchakato wake wa usajili kuwapata wachezaji watakaochezea timu hiyo, mazoezi kwa timu hiyo yanafanyika kila siku asubuhi kupisha michuano ya Kombe la Mwakasonda ambayo yanaendelea kwa sasa kwenye uwanja huo wa Majimaji.

No comments:

Post a Comment