23 July 2012
Mhasibu TRA, wenzake wana kesi ya kujibu
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana imewaona washtakiwa wa kesi ya wizi wa zaidi ya sh. bilioni 3.8 inayomkabili Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Justice Katiti na wenzake wana kesi ya kujibu.
Hakimu Aloyce Katemana, aliyasema hayo wakati kesi hiyo ilipoletwa kwa ajili ya uwamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.
Alisema mahakama hiyo imejiridhisha kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi upande wa mashtaka.
Alidai katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 29, vielelezo 45 na mashtaka 10 yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa.
Wakili wa utetezi Bw. Majula Magafu akizungumza kwa aniaba ya mawakili wenzake, alidai wateja wao watajitetea kwa njia ya kiapo na watakuwa na mashahidi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 23 mwaka huu. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Bw. Samwel Renju, Bw. Haggay Mwatonoka na Bw. Hope Lulandala.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, kati ya Mei na Novemba 2008 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula njama na kuiba fedha za TRA.
Inadaiwa baada ya kufanya wizi huo, washtakiwa walizihamisha fedha hizo katika akaunti za kampuni mbalimbali za watu binafsi wakijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment