23 July 2012

Washtakiwa DECI kujitetea kwa kiapo



Na Rehema Mohamed

WASHTAKIWA wa kesi ya kula njama na kuiba zaidi ya sh. milioni 118 inayowakabili Wakurugenzi wa Taasisi ya Kuendesha na Kusimamia Mchezo wa Upatu (DECI), wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa watajitetea kwa njia ya kiapo.


Washtakiwa hao ni Bw. Dominick Kagendi, Bw. Jackson Mtares, Bw. Timotheo Loitinye na Bw. Samuel Mtares.

Mbele ya Hakimu Stuwart Sanga, wakili wa Serikali Bw. Hamphrey Mariki, alidai kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kuangalia washtakiwa hao watajitetea kwa njia gani.

Wastakiwa hao walidai kuwa, katika utetezi wao hawatakuwa na mashahidi wala kielelezo cha ziada. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 24 mwaka huu, itakapoletwa kwa ajili ya washtakiwa hao kuanza kujitetea.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 16 pamoja na vielelezo mbalimbali. Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja kula njama na kuiba sh. milioni 118,440,000, mali ya DECI kupitia Benki ya Standard Chartered, tawi la Kariakoo.

No comments:

Post a Comment