16 July 2012
Mbunge Dkt. Ndungulile yamkuta bungeni
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndungulile, ametakiwa kuwaomba radhi kuhusu madai aliyotoa kwa madiwani watatu wa jimbo hilo waliokwenda bungeni mjini Dodoma kufuatilia hotuba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuwa wamehongwa na Wizara hiyo.
Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, alitoa amri hiyo baada ya madiwani hao kuwasilisha barua ya kulalamikia madai yaliyotolewa na Dkt. Ndungulile.
Awali katika mkutano wao na waandishi wa habari, madiwani hao walimempa siku saba Dkt. Ndungulile awe awaomba radhi na kama atashindwa kufanya hivyo, hawatashirikiana naye katika kata zao.
Walisema hawewezi kwenda mahakamani ila watakachofanya ni kumnyima ushirikiano katika kata zao hadi atakapowaomba radhi.
Diwani wa Kata ya Vijibweni, Bw. Suleiman Methew, alisema kauli iliyotolewa na mbunge huyo imewadhalilisha kwa wananchi waliowachagua kushika nafasi hizo.
“Sisi tulikuja bungeni kwa fedha zetu na si kwa ufadhili wa mtu yoyote kama anavyodai Dkt. Ndungulile,” alisema.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kibada, Bw. Juma Nkumbi, alisema mbunge huyo amekurupuka kutoa kauli inayosema wananchi wa Kigamboni hawautaki mradi wa kuendeleza mji mpya
Alisema hakuna kikao chochote alichokaa na wananchi, madiwani wala Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambapo maelezo aliyoyatoa ni ya kwake na si msimamo wa wananchi wa Kigamboni.
“Mbunge atajua vipi matatizo ya watu wa Kigamboni wakati yeye mwenyewe anaishi Upanga, wananchi wanasubiria mradi huu ili wapate haki zao,” alisema.
Akizungumzia madai hayo, Dkt. Ndungulile alipinga kauli kuwa yeye hataki mradi huo na kusisitiza anachopinga ni ukiukwaji wa taratibu uliofanywa kutwaa maeneo hayo.
Alisema miongoni mwa maeneo yaliyoonesha udhaifu ni kipengele ambacho kilitaka wananchi wasiendeleze eneo hilo kwa miaka miwili lakini hadi sasa miaka minne hakuna kilichofanyika na wananchi wameshatoa maeneo yao hawajui hatma yao.
Aliongeza kuwa, Wizara hiyo inapaswa kurudi kwa wananchi ili mchakato huo uanze upya na kuodnoa kasoro zilizopona maamuzi hayo yalifanyika kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Temeke Juni 26 mwaka huu na mkutano wa wananchi ambao walimtuma akienda bungeni msimamo uwe ni huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment