17 July 2012
Manji, Sanga, Katabalo kidedea Yanga *Sarah Ramadhan aibukia ukumbini
Na Elizabeth Mayemba
HATIMAYE Klabu ya Yanga imepata viongozi wapya wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi baada ya baadhi ya wajumbe kujiuzulu, ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti mfanyabiashara maarufu nchini Yusuf Manji, ameibuka kidedea huku Makamu wake akiwa Clement Sanga.
Uchaguzi huo ulianza juzi saa 7:30 kwa kila mjumbe kumwaga sera zake kwa wapiga kura, ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji John Mkwawa alitangaza matokeo majira ya saa 10 alfajiri, baada ya kazi hiyo kukamilika.
Kioja ambacho kilitokea katika uchaguzi huo ni pale, Sarah Ramadhan aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo alipovamia jukwaa na kulazimisha Kamati ya Uchaguzi impe nafasi amwage sera zake.
Awali Kamati ya Uchaguzi ya TFF, iliengua jina la Sarah ambaye alikuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti kutokana na kutokuwa na sifa, lakini baada ya tukio hilo alizungumza na waandishi wa habari kwamba anaendelea na kampeni zake kama kawaida na siku ya uchaguzi atahudhuria kama wagombea wengine.
Baada ya kuvamia jukwaa Jaji Mkwawa, aliwaagiza askari ukumbini hapo ili wamtoe nje Sarah kwa madai ya kutaka kuleta vurugu na askari wakafanya kazi yao, lakini cha kushangaza akaenda kukaa sehemu ambayo walikaa wagombea na kugoma kuhama eneo hilo.
Katika kinyang'anyiro hicho nafasi za ujumbe zilikwenda kwa Abdallah Bin Kleb, Aron Nyanda, Moses Katabalo na George Manyama.
Wagombea wote na idadi yao ya kura kwa nafasi ya Mwenyekiti Manji (1876) sawa na asilia 97.0%, John Jambele (40) sawa na asilimia 2.6, Edgar Chibura kura (4) asilimia 0.24.
Nafasi ya Makamu Clement Sanga (1948) sawa na asilimia 62.6 Yono Kevela (475) asilimia 23 na Ayoub Nyenzi (288) asilimia 14.
Nafasi ya Ujumbe Abdallah Bin Kleb (1942), Moses Katabalo (1068), Aaron Nyanda (922), Gerge Manyama (682), Justine Baruti (610), Peter Haule (441) na Beda Tindwa.
Wengine ni Lameck Nyambaya (425), (kura 391), Edgar Fongo (295), Graticius Ishengoma (247), Jumanne Mwamenywa (251), Omary Ndula (170), Ramadhan Said (249) na Yono Kivela (123).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment