16 July 2012
Kesi wa wasomi UDSM yakwama kusikilizwa
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaaam, jana imeahirisha kusikiliza kesi ya inayowakabili wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ya kufanya maandamano na mkusanyiko haramu kutokana na wakili wa Serikali anayeongoza kesi hiyo, Bw. Ladslaus Komanya, kutokuwepo mahakamani.
Wakili wa Serikali Bi. Secilia Mkonongo, alidai mbele ya Hakimu Bi. Waliyarwande Lema, kuwa kesi hiyo ilitajwa kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa, pamoja na wakili huyo kutokuwepo, washtakiwa watatu kati ya hao hawakuwepo mahakamani kutokana na sababu mbalimbali. Kesi hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13 mwaka huu.
Awali ilidaiwa kuwa, Novemba 14 mwaka huu, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza wakidaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo la chuo.
Ilidaiwa kuwa, washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka watawanyike lakini walikahidi amri hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment