23 July 2012
JK: Siasa za chuki majibu yake 2015
Na Waandishi Wetu, Mbeya
RAIS Jakaya Kikwete amesema wanasiasa wanaotangaza siasa za chuki na migogoro badala ya kutangaza maendeleo kwa Watanzania, wasubiri mwaka 2015 ili wapate majibu ya kazi wanayoifanya.
Alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao kila kukicha wantangaza migogoro na chuki miongoni mwa Watanzania na kusahau kuwa, wanchotakiwa kufanya ni kutimiza ahadi walizotoa katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Rais Kikwete aliyasema hayo mjini Mbeya jana wakati akihutubia umati mkubwa wa watu baada ya kuzindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira uliogharimu zaidi ya sh. bilioni 74 ambapo Tanzania imechangia sh. bilioni 29.
Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Ujeruman, Jumuia ya Ulaya na Mfuko wa Maendeleo ya Maji Mijini jijini Mbeya ambao upo kwenye Kijiji cha Swaya.
“Wakati CCM inazungumzia maendeleo katika nchi yetu, wapo wanasiasa ambao kila kukicha wanatangaza migogoro na chuki miongoni mwa Watanzania badala ya kutekeleza ahadi walizotoa.
Alionya watu wenye tabia ya kuchezea vyanzo vya maji waache mara moja kutokana na rasilimali ya maji nchini kupungua siku hadi siku hivyo kufanya iliyopo itunzwe vizuri.
“Maji haya yanufaishe watu wote bila kujali itikadi zao kidini na kivyama, mimi ni rais wa nchi hivyo jambo la msingi kila Mtanzania atunze rasilimali hii ambayo ni muhimu sana,” alisema.
Alisema maandamano yanayofanywa na baadhi ya vyama vya siasa nchini, yameanza kumkera ambapo baadhi ya matamko ambayo yanatolewa katika maandamano na mikutano, yana lengo la kuvuruga amani na kuchochea vurugu.
Aliongeza kuwa, mradi huo una uwezo wa kutoa lita za maji milioni 51.8 ambapo mahitaji yaliyopo kwa sasa jijini hapa ni lita milioni 38 na una uwezo wa kutoa huduma kwa miaka mitano ijayo.
“Huu mradi ni mkubwa, una uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wananchi hadi mwaka 2017, Wizara ya Maji iweke mikakati endelevu kwa mahitaji yajayo.
“Wanawake wanasumbuka muda mrefu kusaka maji na kusababisha baadhi ya ndoa kuyumba..sasa naamini ndoa zenu zitaimarika kwa kuwa maji safi na salama yanapatikana,” alisema.
Balozi wa Ujeruman nchini, Bw. Klaus Peter Blandes, alisema nchi yake imefarijika na mradi huo ambao umeimarisha uhusiano ulioopo kati yao na Tanzania hivyo wananchi wanapaswa kuutunza ili kumaliza tatizo kubwa la maji jijini hapa.
Kamishna wa Maendeleo wa Jumuia ya Ulaya, Bw. Andris Piebalgs, alisema mradi huo ni mwendelezo wa msaada wake kwa Tanzania utawasaidia zaidi ya watu 400,000 kupata maji safi muda wote.
“Jumuiya imekuwa ikitoa euro milioni 100 kwa ajili ya maendeleo
nchini Tanzania hivyo mradi huo, utawafanya Watanzania hasa waishio jijini hapa kuwa na uhakika wa kupata maji.
Habari hii imeandikwa na Charles Mwakipesile, Rashid Mkwenda na Esther Macha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

ndiyo tusubiri hiyo 2015 ukweli uje kujulikana
ReplyDeleteJoshua
ReplyDeleteHaya mkuu wa nnchi umeyataka mwenyewe na sasa unaona yakuzidi nguvu ndo maana hata watoto wa vigogo wanatumia technologia ya kuweza kutumia mtandao wa mtu wa cm na kutuma sms kwa kutumia namba ya mhusika bila ya mhusika kujua
Kaka subiri 2015 watanzania wenye akili watatoa majibu nunue kanga na kofia za kutosha kwa kazi hiyo
Ni vyema raisi wa nchi akatumia busara zaidi kuliko vijembe ambavyo havina nafasi kwa maendeleo ya nchi. Ni bora akawa mzalendo kwa kufanyia kazi hoja zote zitolewazo na wabunge haswa wa upinzani kwani zina mashiko na maslahi ya nchi. Mzalendo wa kweli hufanyia kazi mambo yanayolenga kuleta maendeleo ya Taifa lake
DeleteCCM IPENDEKEZE MGOMBEA ANAYOUZIKA SI VIZURI KUWAPA UPINZANI HOJA ZA KUJINASIBU CCM IACHE MARA MOJA KUIMBA WIMBO WA UPINZANI WABUNGE WA CCM WAACHE KUWASAIDIA UPINZANI KUKOSOA CHAMA TAWALA SI UTARATIBU
ReplyDeletempinzani wa ccm atatoka ndani ya ccm.mwl.jk nyerere. cdm.cuf.na wengine bado hawajaosha uwezo wa kuongoza hata watu 50 ni ubinafsi udini na ukanda na uchochezi ndio sera zao, kama wapinzani waukweli wabadilike waachane na hizo sera
ReplyDeletehahahaha JK unachekesha na siasa zako chuki, how about SIASA ZA KIFISADI? na jinsi zilivyotufikisha hapa tulipo? Watanzania wana haki ya kuchukia na kuwachukia MAFISADI
ReplyDelete