10 July 2012

Jalada ya kesi ya Lulu latakiwa mahakama ya rufaa


Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewataka upande wa mashtaka katika maombi ya kupinga umri wa mshtakiwa wa kesi ya Mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini Elizabert Michael 'Lulu' kuhakikisha jalada la kesi hiyo linapelekwa Mahakama ya Rufaa.

Jaji anayesikiliza maombi ya kupinga umri wa msanii huyo Dkt. Fauz Twaib aliiambia mahakama jana kuwa tayari Mahakama ya Rufaa imeshapeleka barua mahakamani hapo kuomba faili la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa maombi ya kupinga umri wa msanii huyo na imeahirishwa hadi Julai 23 mwaka huu.

Awali maombi hayo yalipangwa kusikilizwa Juni 25, mwaka huu lakini ilishindikana baada ya Wakili wa serikali Elizabeth Kadanda kuiomba  Mahakama hiyo kuahirisha au kusitisha kusikiliza maombi hayo kwasababu wamewasilisha maombi mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa jaji huyo.

Uamuzi uliopingwa ni ule aliutoa Juni 11, mwaka huu wa kukubali kusikiliza maombi ya kuchunguza umri wa Lulu ili kujua umri wake halisi baada ya kuwa na utata upande wa mashitaka unaodai Lulu ana miaka 18.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

1 comment:

  1. ASAMEHEWE COZ UKWELI WA KIFO ANAUJUA MAREHEMU

    ReplyDelete