11 July 2012
Filamu za Kanumba zawatia kiwewe mashabiki
Na Amina Athumani, Zanzibar
WADAU na mashabiki wa filamu nchini, waliofika kushuhudia tamasha la filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF), wamepata shauku ya kuziona filamu za marehemu Steven Kanumba.
Filamu za Kanumba pamoja na wasanii wengine wa Tanzania zinatarajia kuoneshwa Julai 14, mwaka huu ambazo zimetengewa kuoneshwa kwa siku nzima, tofauti na filamu nyingine kutoka nchi nyingine za majahazi.
Wakisikika wadau hao ambao walijitokeza jana wakati wa kuoneshwa filamu ya Fantasy, Papanzenu na 35 and Ticking zote za kigeni walisikika wakisema wangependa kuiona filamu ya This is It, ambayo imekuwa ikitanjwa kila kona ya Ngome Kongwe.
Wengi walidai hawakuwa wakimfahamu Kanumba kupitia filamU zake zilizopita isipokuwa wamemfahamu zaidi kupitia filamU ya This is It ambayo, imekuwa ikipendwa zaidi na watoto.
Kanumba ambaye ni mdau mkubwa wa tamasha hilo amekuwa akihudhuria kila mwaka katika tamasha hilo, ambapo tayari ameweza kutwaa tuzo mbalimbali za ZIFF kupitia tamasha hilo.
Kwa mwaka huu waandaaji wa ZIFF, wameandaa tuzo maalumu ya Kanumba Award ambayo itatolewa Julai 15, mwaka huu kama sehemu ya kukumbuka mchango wa msanii huyo.
Pamoja na Kanumba Award, tuzo nyingine zitakazotolewa ni filamu bora, mtayarishaji bora, muongozaji bora, msanii bora, Signis Jury, Verona Jury, Osumane Sembene na tuzo nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment