Na Mwandishi Wetu
FINALI ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayozikutanisha timu za Mwanza na Morogoro itachezwa leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kuanza saa 9 alasiri.
Katika michuano hiyo, Mwanza ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Temeke mabao 3-1.
Nayo Morogoro imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Tanga kwenye nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1.
Mechi zote za nusu fainali ya michuano hiyo iliyozikutanisha timu za vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini zilichezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Temeke na Tanga, itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 5 asubuhi.
Mashindano hayo ya Copa Coca-Cola 2012, yalianza Juni 24 mwaka huu yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment