23 July 2012

EAC yataka mkataba wa kudhibiti biashara, usafirishaji silaha



Na Nicodemus Ikonko, EANA

MAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich, amesema jumuiya hiyo ingependa kuwepo Mkataba wa Biashara ya Silaha (ATT) ambao utadhibiti usafirishaji haramu wa silaha.

Dkt. Rotich aliyasema hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Maofisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), juu ya mkataba wa ATT mjini New York, nchini mwishoni mwa wiki.

“Nchi za EAC zingependa kuona mkataba wa ATT, ambao utashugghulikia matatizo ya usafirishaji sialaha haramu katika nyanja zote, uhakika wa kuheshimu utaifa na mipaka ya nchi,” alisema Dkt. Rotich.

Aliongeza kuwa, uzoefu ulioupata kwenye Kanda ya EAC, unaonesha maafa makubwa yanayotokana na usafirishaji haramu wa silaha ambao hivi sasa unapaswa kudhibitiwa kisheria.

Alisema upatikanaji kirahisi wa silaha haramu, unachangia mambo mengi ya watu kutawanyika, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uzalilishaji Serikali zilizochaguliwa na wananchi.

“Uhusiano kati ya usafirishaji haramu wa silaha, haki za binadamu na masuala ya kibinadamu ni mambo muhimu ambayo hayana budi kuwemo kwenye mkataba,” alisema

No comments:

Post a Comment