16 July 2012
Cheka, Nyilawila kuzichapa Sept. 29
Na Zahoro Mlanzi
MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka na Karama Nyilawila, wanatarajia kupanda ulingoni Septemba 29, mwaka huu kuwania ubingwa wa Chama za Ngumi za Kulipwa (PST), katika pambano litakalofanyika PTA, Dar es Salaam.
Wakizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, mabondia hao walisema wamekubali kucheza pambano hilo siku hiyo baada ya mkanda wa ubingwa huo kuwa wazi na litakuwa la raundi 12.
Cheka alisema anaendelea na mazoezi juu ya pambano hilo na kwamba mpinzani wake anamjua vizuri, hivyo hana tatizo naye zaidi ni kusubili siku hiyo.
"Ni kweli nimekubali kucheza na Karama kwakuwa tunawiana kwa baadhi ya hususani katika rekodi za mapambano yake na yangu, hivyo ninajiandaa kwa ajili ya kuendelea kuweka heshima nchini," alitamba Cheka.
Naye Nyilawila alisema amekuwa anapata wakati mgumu kila anapokutana na Cheka lakini hivi sasa amejipanga vizuri kuhakikisha anamchapa na kutwaa ubingwa.
Kabla ya pambano hilo, litatanguliwa na mapambano sita ya utangulizi ambayo kila moja litakuwa na raundi sita ambapo Seba atapigana na Stam Kess katika uzito wa kila 66.
Pia kutakuwa na pambano la Cosmas Cheka atacheza na Fadhili Hawazi, Juma Kihiyo na Ibrahim Mahokola, Hassan Kidebe ataoneshana kazi na Deo Samwel, Anthony Mathias atazichapa na Shaaban Kilumbe na Amos Mwamakula atapigana na Sadick Momba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment