16 July 2012
CHASHUBUTA wapata viongozi wapya
Na Benard Bugoma
CHAMA cha Shule Binafsi za Udereva nchini (CHASHUBUTA), hivi karibuni kimefanya uchaguzi wa kwanza wa viongozi wake ngazi ya Taifa ambao watakaa madarakani kwa miaka mitatu.
Uchaguzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na kujumuisha wajumbe kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara ambayo ni Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Iringa.
Nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ilichukuliwa na Bw. Robert Mkolla ambaye ni Mkurugenzi na mmiliki wa shule ya udereva ya Future World Driving School iliyopo Buguruni.
Akizungumza na Majira, Bw. Mkolla alisema lengo la kuanzisha chama hicho ni kuziunganisha shule binafsi za udereva ili waweze kuwa na sauti ya pamoja katika kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya kupambana na ajali za barabarani nchini.
Alisema viongozi wote waliochaguliwa watakaa madarakani hadi Julai 6,2016 ambapo nafasi ya Mwenyekiti Msaidizi ilichukuliwa na
Bw. Hua Tluay Matia, ambaye ni mmiliki wa Shule ya Udereva ya Hua Driving School iliyopo Mabibo Dar Es salaam.
Katibu Mkuu, Bw. Jonas Bigaye Mhati (Mkurugenzi na mmiliki wa shule ya New Vision VTC Driving School) na Katibu Msaidizi Bw. Erasmus Mapunda (Mkurugenzi na mmiliki wa Tumaini VTC Driving School Kimara Suka Dar es Salaam).
Wengine ni Mhasibu Mkuu, Bw. Delphiner Costantine (Mmiliki na Mkurugenzi wa COSTEFATHA Driving School, iliyopo Mwenge Dar es Salaam) na Mhasibu Msaidizi Bw. Mathew Guzzo (Mmiliki wa Gift Driving School, iliyopo Tabata Dar Es Salaam).
Bw. Mkolla aliwataja wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji ambao ni Bw. Cleti Lammers, kutoka Morogoro Mjini, Bw. Deograsias Msaki (Arusha Mjini), Bw. Juma Mangu (Mwanza Mjini), Bw. Cosmas Munuo (Kilimanjaro), Bi. Fridah Mwakyusa (Mbeya Mjini), Bw. Ondi Nyalari, kutoka Dodoma Mjini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment