17 July 2012
BTL Queens yatwaa Bandari Chalenji Cup
Na Elizabeth Mayemba
TIMU ya netiboli ya Kampuni ya Business Times Limited (BTL Queens), imetwaa ubingwa wa Bandari Chalenji Cup baada ya kuichapa Bandari B kwa mabao 37-21.
Mchezo huo ulifanyika jana jioni kwenye Uwanja wa Habours, Dar es Salaam ambapo michuano hiyo iliendeshwa kwa mtindo wa ligi.
Kwa kutwaa ubingwa huo, TBL Queens ilipewa zawadi ya kikombe, cheti, jezi seti mbili na fedha taslimu sh. 300,000 huku Mwandishi wa gazeti hili (Elizabeth Mayemba) aliibuka mwandishi bora wa michuano hiyo.
BTL Queens ilitwaa kombe hilo baada ya kushinda mechi zake katika ligi hiyo ambapo ilizifunga Jeshi Stars, Bandari A kwa nyakati tofauti.
Mratibu wa michuano hiyo, Ken Mwaisabula alizishukuru timu zote zilizoshiriki michuano hiyo na kuipa pongezi za pekee BTL Queens kwa changamoto iliyoleta katika michuano hiyo.
Kampuni hiyo ndio inayochapisha gazeti hili pamoja na Spoti Starehe na Business Times.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment