16 July 2012
Asasi yajipanga kupunguza umaskini Angelina Mganga na Ester Paul
ASASI ya Building Afrika ipo katika mkakati wa kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania ili kusaidia kufikiwa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2015.
Mwenyekiti wa asasi hiyo, Bw. Deogratias Celestine, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya asasi hiyo katika kufikia malengo ya milenia na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA)
Kwa upande wale Dkt. Peter Kibacha, alisema malengo ya milenia ni Tamko la Umoja wa Mataifa (UN), ambayo yanatakiwa kuwa yamefikiwa ifikapo mwaka 2015.
Aliongeza kuwa malengo hayo ya milenia ni kupunguza umaskini uliokithiri, elimu kwa wote usawa wa kijinsia, kupunguza vifo vya watoto, kuboresha afya ya uzazi, kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI, malaria, kisukari na mengine.
Kwa upande wa Bw.Mhegelele Mhuda, alisema malengo ya MKUKUTA ni pamoja na kukuza utawala bora na uwajibikaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment