02 July 2012

Afrika inamalizwa na migogoro ya udini, visasi


TATIZO la ugaidi ni janga ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiutikisa ulimwengu kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Tatizo hilo lilianza kushika kasi miaka ya 1990 baada ya mwaka 1998 kufanyika mashambulizi katika Balozi za Marekani  nchini Tanzania na Kenya kabla ya kufuatiwa na shambulizi kubwa lililofanyika Septemba 11, 2001.


Katika shambulio hilo magaidi 19 wenye uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaida waliteka nyara ndege nne za abiria ambazo zilikuwa njiani kwenda  California, zikitokea kwenye viwanja tofauti vya ndege Mashariki mwa Marekani.

Tangu kipindi hicho yameshuhudiwa mashambulizi mbalimbali ambayo yamekuwa yakizitikisa nchi za Mashariki ya Kati na nchini za Magharibi.

Miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikilengwa zaidi ni Marekani na Uingereza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa mstari wa mbele kukomesha mtandao huo.

Tatizo hilo limekuwa likisababisha wingu la wasiwasi kutanda katika  mataifa hayo huku yakiyashutumu baadhi ya mataifa ya kiarabu kwa kufadhiri mitandao hiyo.

Hali hiyo  ilizilazimu baadhi ya nchi  katika ukanda huo kujitosa katika vita dhidi ya mtandao iliyofanikisha kuuawa kwa kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda,Bw.Osama Bin Laden.

Nigeria ni miongoni mwa nchi ambazo zimejikuta zikikabiliwa na tataizo hilo ambapo imeshuhudiwa mamia ya watu wakipoteza maisha huku wananchi wakiishi kwa mashaka kutokana na vurugu za kila siku zinazoongozwa na kundi la Boko haram.

Boko haram kwa maana yake elimu za magharibi ni dhambi,  kilianza harakati zake mwaka 2003 na mwaka mmoja baadae kilifanya shambulio la kwanza.

Wanamgambo hao huvaa mavazi yanayofanana na kikundi cha Taliban wakifunga vilembe kichwani na kufuga ndevu nyingi.

Madai ya kundi hilo ni kutaka kuanza kutumika sheria ya dini ya kiislamu, shariah, katika taifa zima la Nigeria lenye lenye waislamu na wakristo.

Mwaka 2009, kiongozi wa zamani wa kundi hilo, Bw.Mohammed Yusuf, alipigwa risasi akiwa mahakamani na kuuwawa baada ya kusabisha mauwaji ya watu 800 katika mapigano na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

Matukio hayo yaliifanya serikali ya Nigeria kuanza kupambana nao ambapo, kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau akizungumzia kauli hiyo alisema Rais Jonathan hawezi kuwafanya lolote na hawaogopi kufa."

Mei 2 mwaka huu, mtu mwingine mwenye silaha aliwauwa watu 56 katika mji wa Potiskum, katika jimbo la Yobe, ambapo polisi wa jimbo hilo walithibitisha vifo vya watu hao na kulihusisha tena kundi la Boko Haram.

Bomu la kujitolea mhanga kanisani liliripuka tena katika mji wa Yelwa, karibu na viunga vya Bauchi, Juni 3. Siku saba baadae watu watatu wenye silaha waliwapiga risasi waumini wa kikristo waliokuwepo kanisani katika mji wa Biu jimbo la Borno.

Mauaji mengine yalifanywa Januari 2012 katika eneo la Kano, na kusababisha watu 186 kufariki. Shambulio hilo lilitanguliwa na shambaulio lingine katika makazi ya Umoja wa Mataifa, Abuja na kusababisha vifo vya watu 23 agosti mwaka 2011.

Mji wa Kaskazini wa Nigeria Kano umekuwa ukifanya kila jitihada kurejesha hali ya kuaminiana baina ya jamii na waislam na wakristo, licha ya vitisho vya kigaidi vya Boko Haram.

Katika hali isiyo ya kawaida wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Boko Haram walivishambulia vituo kadhaa vya serikali kwa kuvirushia mabomu na kuwapiga risasi askari polisi.

Zaidi ya watu 180 waliuwawa katika mji huo ambao ni  wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria hali iliyofanya wananchi kupewa hadhari ya kutoka nje usiku.

Miezi michache baadae hali ya kawaida ingawa baadhi ya majimbo yalianza kupata hofu kutokana na mashambulio dhidi ya makanisa na dhidi ya vikosi vya usalama.

Kano ni jiji la kale ambalo wakazi wake ni waislamu, lakini tangu enzi za ukoloni wahamiaji wa kikristo walihamia huko kutoka sehemu ya kusini ya Nigeria.

Mbali wa Igbo ambao ni wakristo, katika mtaa huo wa Sabo Gari wanaishi pia watu wa kabila la Yoruba kutoka eneo la kusini magharibi la Nigeria ni waislamu.

Maisha yao yamekuwa ya mashaka kutokana na kubaguana kupitia dini ambapo makananisa yamekuwa yakichomwa moto na kuua wananchi wasio na hatia.

Kutokana na hali hiyo linaposikika suala la udini ni wazi kuwa watu hao hawawezi kushirikiana katika jambo lolote na kusaha kuwa kuna nguvu kutoka nje inayochochea vurugu hizo.

Vitendo hivyo vimekuwa vikiitesa sana Nigeria kisiasa na kiuchumi kwani imefika wakati kila dini kutaka kuwa na kiongozi wake, hali hii ni mwanzo kutokuwepo amani.

Yanayotokea leo Nigeria yawe somo katika nchi nyingine ikiwemo Tanzania kwani ubaguzi ni tatizo linalosababisha dhambi nyingi na kuzaa migogoro isiyoisha.

"Wananchi wanapobaguana kwa kigezo cha dini hawawezi kuaminiana wala kufanya naye shughuli yoyote ya maendeleo,"

Kumekuwa na migogoro endelevu Afrika hali inayozidi kuliyumbisha na kuongeza umaskini kwa nchi hizo kutokana na viongozi wengi kutumia muda mrefu kumaliza matatizo yanayojitokeza badala ya kupanga miradi ya maendeelo.

Viongozi hawatakiwi kuifumbia macho migogoro ya kidini bali kupitia Umoja wa Afrika ili kuondoa mazingira yanayoweza kupelekea maafa makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamau.

Kwa miaka mingi sasa, dhana ya udini na ukabila ilikuwa moja na tatizo sugu lililowatesa waafrika wakijikuta wanaangukia katika mauaji na kuanza kuibuka baada kuanzishwa kwa uasi katika serikali zao.

Katika hili Umoja wa Afrika umekuwa ukishindwa kusulihisha migogoro hii kwa kukosa mamlaka kutokana na misaada inayokuja na masharti wanayopewa kuendeleza umoja huo.

Umaskini uliopo umesabishwa kwa kiasi kikubwa na migogoro na misaada ya wahisani amabyo hutolewa kwa kuelekeza katika kile wanachopanga wao.

Magonjwa na njaa pia ni athari ya migogoro hiyo kutokana na shughuli nyingine ikiwemo uzalishaji wa chakula kusimama kwa hofu ya wananchi kuathiriwa na vita hiyo.

Mashambulizi katika makanisa yanatakiwa kukomeshwa mara yanapoibuka ili kuepusha hasira na malumbano baina ya pande mbili.

Uasi hutokana na kutoelewana miongoni mwa viongozi ambao hushindwa kuafikiana na kuanza kuipinga seriakali yao huku wakipata msaada wa silaha na fedha kusikojulikana.

Hatupendi kufikia huko baada ya matukio ya hivi karibuni ya kuchoma makanisa bali usuluhishi ufanyike na kuyakemea yasijirudie.

Imeandaliwa na Godfrida Jola kwa msaada wa Mashirika

1 comment:

  1. MATATIZO YANAYOZIKUMBA NCHI ZA ULIMWENGU WA TATU KUSHINDWA NI KUSHINDWA KUCHUJA MAZURI NA MAPUNGUFU YA UTANDAWAZI WAO YAYOWAVUTIA KUYAPA KIPAUMBELE NI MAPUNGUFU KUTOKANA NA UELEWA FINYU WA UTANDAWAZI

    ReplyDelete