LIBREVILLE, Gabon
NAHODHA wa timu ya taifa ya Mali, Cedric Kante amesema walistahili kushinda mechi yao ya robo fainali, dhidi ya waandaaji wenza Gabon kutokana na morali waliyokuwa nayo.
Hadi muda wa nyongeza unamalizika, timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na Mali ikafanikiwa kusonga mbele kwa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa njia ya penalti, baada ya kiungo wa Barcelona, Seydou Keita kupachika bao lililoihakikishia ushindi timu hiyo.
"Nimefurahi sana, ulikuwa ni mchezo wa ajabu," Kante aliiambia BBC Sport.
"Japokuwa ni uendawazimu kwa kushinda kwa mikwaju ya penalti, lakini nadhani tulistahili kushinda," alisema.
Katika mchezo huo wa juzi, Gabon ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Eric Mouloungui ambaye pia aligonga mwamba mara mbili, lakini kikosi hicho cha Alain Giresse kikapigana na kutoka nyuma baada ya mchezaji aliyetokea benchi, Cheick Diabate akapachika bao dakika ya 84.
“Kuna historia kubwa katika soka la nchi hizi mbili, mashabiki wetu wataendelea kutushuhudia na wangependa tuifunge Ivory Coast,” alisema nahodha huyo.
Alisema japokuwa walizikosa nafasi mbili za kufunga, lakini walicheza soka la hali ya juu.
Kante vilevile anaamini kuwa ubora wa kikosi chao, ndiyo msingi mkuu wa ushindi huo.
No comments:
Post a Comment