06 July 2012

15 wateuliwa kuchezesha Kombe la Kagame



Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14 hadi 28 mwaka huu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilieleza kuwa waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu.

Wambura alisema waamuzi hao wanatakiwa kuwasili mapema kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.

Alisema kwa upande wa waamuzi wa kati walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Wambura aliwataja wamuzi wasaidizi kuwa ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Chang'walu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).


No comments:

Post a Comment