01 June 2012

Msondo Ngoma kuzindua Emirates



Na mwandishi wetu

BENDI kongwe ya muziki wa dansa nchini, Msondo Ngoma ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya wa burudani wa Emirates uliopo Masasi, Mtwara Juni 2 mwaka huu kwa lengo la kufanya shoo zao.

Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo, ambapo wamepania kutoa burudani ya nguvu.

"Unajua sisi ni Baba ya Muziki nchini, ndiyo maana wapenzi wengi wa dansi wanahitaji burudani kutoka kwetu, tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kufanya kazi ya nguvu," alisema Super D.

Alisema siku hiyo wanatarajia kupiga vibao vyao vya zamani na vipya kwa lengo la kuwakumbusha wapenzi wa bendi hiyo nyimbo zao, ambazo zilitamba na kupendwa katika tasnia ya muziki wa dansi.

Alivitaja baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu uliotungwa na Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi (Juma Katundu) na Baba Kibene (Eddo Sanga).

No comments:

Post a Comment