14 May 2012

Waislaamu watakiwa kupuuza wanapinga sensa



Na Anneth Kagenda

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kiislam ya  Peace Foundation Tanzania (TIPF), Bw. Sadiki Godigodi, amewataka Watanzania kupuuza ushawishi unaotolewa na baadhi ya watu wa dini hiyo wa kuwataka wasishiriki kwenye sensa kwani hakuna nchi ambayo inaweza kukaa bila kujua idadi ya wananchi wake.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema kuwa ni muda muafaka kwa waumini wa dini hiyo kutosikiliza ushawishi unaotolewa na baadhi ya watu badala yake wakubali kushiriki vyema kwenye sensa hiyo.

"Tunawaomba waislam, wakristo na Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kutoa ushirikiano wa zoezi la kuhesabu watu na makazi linalotarajia kuanza hivi karibuni na wapuuze kauli za watu wachache wenye malengo ya kujipatia maslahi binafsi," alisema.

Alisema watu hao ambao wamekuwa wakishawishi wenzao kutoshiriki Sensa ni kikuzwa, kwani hii ni fursa muhimu.

Katika hatua nyingine (TIPF) ilimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua yake ya kusikiliza mawazo ya wabunge na badaye kuchukua hatua mbadala ya kuwawajibisha wale wote walioonekana kuwa si waadilifu kwenye Baraza la Mawaziri.

"Kwanza kabisa taasisi yetu inapenda kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa kusikia kilio cha wabunge hatimae kuwawajibisha mawaziri wenye kashfa za ufisadi.


No comments:

Post a Comment