03 May 2012
Vyama vyenye upinzani mkali
VYAMA vyenye upinzani mkali kisiasa vya CHADEMA na CCM kila kimoja kimeibuka na ushindi katika kesi za kupinga matokeo yaliyowapa ushindi wabunge wa vyama hivyo katika majimbo ya Segerea, jijini Dar es Salaam na Mbozi Mashariki, mkoani Mbeya.
Katika Jimbo la Segerea, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kesi ya kupinga uchaguzi wa Dkt. Makongoro Mahanga (CCM) iliyokuwa imefunguliwa na mpinzani wake wakati wa uchaguzi wa 2010, Bw. Fred Mpendazoe.
Kwa upande wa Jimbo la Mbozi Mashariki Mahakama ya Rufaa Kanda ya Kusini, iliyoketi jana jijini Mbeya ilitupilia mbali rufaa iliyokatwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dkt. Lucas Siyame, akipinga ubunge wa, Bw. David Silinde.
Wakitoa hukumu ya kesi hiyo No. 24 ya mwaka 2011, jana, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Kanda ya Kusini, wakiongozwa na Jaji Msofe, wameondoa shauri hilo mahakamani hapo baada ya upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake kuiambia mahakama kuwa hauna haja na kesi hiyo tena.
Kufutia hatua hiyo jopo hilo la majaji wa Mahakama ya Rufaa likikubaliana na hoja iliyotolewa na upande wa utetezi na limemwamuru mlalamikaji kulipa gharama za shauri hilo tangu ngazi ya Mahakama Kuu.
Kwa upande wake Dkt. Mahanga, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitupilia mbali hoja 11 zilizowasilishwa na upande wa madai kupinga ushindi wa mbunge huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment