03 May 2012
Arusha wazidi kuichoka CCM
Na Sophia Fundi, Arusha
MZIMU wa CCM kukimbiwa na wanachama wake na kujiunga na CHADEMA umeendelea baada ya wanachama 70 kukihama chama hicho.
Wanachama waliohama chama hicho ni wa Kata ya Endulen iliyopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mbunge wa Jimbo la Karatu, Bw.Izrael Natse jana aliwataka viongozi wa CCM kuacha kuwatisha wananchi wanaohama na kujiunga na CHADEMA.
"Viongozi wa CCM acheni kuwatisha wananchi watumie demokrasia yao kujiunga na CHADEMA, wameona inafaa na wamechoka kukaa na mafisadi," alisema.
Bw.Natse alisema CHADEMA ni chama pekee cha kisiasa nchini kilicho na malengo ya kweli ya kuwaletea mabadiliko Watanzania na ndiyo maana kimekuwa kikikubalika na kuaminiwa na wananchi kwa kasi ya aina yake.
Aliwahimiza wananchi wa Kata Endulen wilayani Ngorongoro, ambapo ndipo ngome ya CCM kuacha uoga na kujitokeza kwa wingi kurudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA.
"Wananchi wenzangu njooni, rudisheni hizo kadi za CCM msiwe na woga hakuna atakayewafanya kitu tumieni demokrasia," alisisitiza Bw.Natse.
Pia aliwashauri wakazi wa Kata ya Endulen kuiga mfano kwa majirani zao wa Karatu waliokataa CCM na kumchagua mbunge na madiwani wa kutoka CHADEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment