LONDON, England
BAADA ya kuifungia timu yake ya Chelsea mabao matatu dhidi ya QPR, mshambuliaji Fernando Torres amesema kwamba watarajie makubwa kutoka kwake.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mabao hayo yaliifanya Chewlsea juzi kuibuka na ushindi wa mabaoa 6-1, yamekuja ikiwa ni baada ya kuisadia timu hiyo kwenye Uwanja wa Nou Camp .
Akizungumzia kuhusu mabao hayo, Torres ambaye anatarajia kuiongoza timu hiyo dhidi ya timu yake ya zamani ya Liverpool katika mechi ya fainali kuwania michuano ya Kombe la FA, alisema kwamba ni matokeo mazuri kwake na anayafurahia na ana matumaini ya kwamba ndiyo ya kwanza katika makubwa atakayoyafanya.
"Msimu huu ulikuwa ni mbaya, sikuwa na matokeo mazuri na yalimfanya abadilishwe kocha katikati mwa msimu.
"Hakuna mtu hata mmoja ambaye alituunga mkono, lakini kwa sasa tuna matumaini ya kumaliza tukiwa nafasi nne za juu na kama ungeweza kumuuliza mtu nusu ya kwanza msimu huu hakuna aliyeipa nafasi Chelsea, lakini kwa sasa kila mmoja anatupongeza," alisema mchezaji huyo.
Alisema pamoja na ushindi, lakni kesho bado wanakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Newcastle na mechi hiyo ndiyo muhimu kwao ni lazima washinde, ili waweze kutinga nafasi ya nne bora.
"Tutakuwa karibu kutinga hatua ya nne bora na kama tutashinda mechi hiyo, tutaelekeza nguvu zetu katika mechi ya fainali ya Kombe la FA, tukiwa na morali kwa hiyo wiki hii ni muhimu kwetu," alisema Torres.
Mbao hayo matatu ni ya kwanza kwa Mhispania huyo tangu mwaka 2009 na anatarajia kuumaliza akiwa mshambuliaji tofauti na kama ilivyokuwa mapema msimu huu.
No comments:
Post a Comment