02 May 2012

Hodgson aomba kuungwa mkono na mashabiki

LONDON, England

KOCHA Roy Hodgson amewaomba mashabiki wa timu ya taifa ya England, kumuunga mkono baada ya Chama cha Mpira wa Miguu nchini humo (FA) kumuomba kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Hodgson (64), ndiye kocha pekee ambaye ameombwa na FA ambapo jana yalikuwa yafanyike makubaliano ili kukabidhi mikoba hiyo iliyoachwa na kocha Fabio Capello.

Hata hivyo Hodgson, ambaye alitimuliwa na  Liverpool miezi 16 iliyopita na amabye anaomba kuungwa mkono na mashabiki ili aweze kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa Ulaya Euro 2012, alisema anatarajia kukubali wadhifa huo.

Msimu huu kocha huyo aliiambia SunSport: "Nina matumaini endapo nitapewa kazi ya kuinoa England, itahitaji kuungwa mkono na watu muhimu ambao ni mashabiki na vyombo vya habari.

"Itakuwa ni kazi ngumu kwa kila mtu ambaye haungwi mkono.

"Hata kama una uwezo na labda ni haki ya mtu, unahitaji kujua kama haki ya mtu. Ni muhimu kuungwa mkono," alisema kocha huyo kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

Hodgson, ambaye amewahi kuzinoa timu za Switzerland, Falme za Kiarabu na Finland, pia alipongezwa na kocha wa Tottenham, Redknapp.

"Ni bahati nzuri kwa Roy. Nitaangalia hatima yangu Tottenham na ningependa kubaki na timu hiyo, lakini jambo hilo lipo chini ya Mwenyekiti," alisema kocha huyo.


No comments:

Post a Comment