10 May 2012
Sekta zashauriwa kutoa ajira bila ubaguzi
Na Heri Shaaban
WAZIRI wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana Bi.Gaudensia Kabaka amezishauri sekta mbalimbali za kutoa ajira bila ubaguzi, sambamba na kuwataka watumishi kutoa kipaumbele kwa suala la ajira kwa walemavu.
Ushauri huo uliutoa Dar es Salaam jana,na Waziri wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana Bi.Gaudensia Kabaka katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha Televisheni
Bi.Kabaka alisema kuwa watumishi wengi wameshindwa kuwapa kipaumbele walemavu wanapoomba nafasi za kazi badala yake wanaangalia mtu alivyo.
"Imegundulika kuwa watumishi wengi katika maombi ya kazi wanashindwa kuwapa kipaumbele walemavu wanapoomba ajira za Serikali jambo ambalo wizara yangu inalipinga kwa asilimia kubwa ,"alisema Bi.Kabaka
Pia alisema kuwa zaidi ya Watanzania 450 wapo nchini Uharabuni katika ajira mbalimbali ambapo wizara imetoa idhini ya kufanya kazi katika nchini hiyo.
Aliongeza kuwa Wizara ya Kazi na Ajira inatarajia kujifunza mbinu inayotumika Kenya kupata ajira kwa watu wake ili Watanzania waweze kunufaika na waweze kuajirwa sehemu mbalimbali za nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment