17 May 2012
Marekani yaahidi kusaidia kumaliza tatizo la umeme
NA MICHAEL SARUNGI
UBALOZI wa Marekani nchini umetaja mikakati mbalimbali ambayo Tanzania inatakiwa kutumia kukabiliana na tatizo sugu la umeme na kuahidi kusaidia eneo hilo.
Mikakati hiyo ilitajwa Dar es Salaam jana katika mkutano uliowakutanisha mawaziri wa Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wa ubalozi wa Marekani ulioongozwa na balozi wa nchi hiyo nchini, Bw.Alfonso Lenhardt.
Bw. Lenhardt katika mkutano huo alisema nchi yake ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha tatizo hilo linakuwa ni jambo la kihistoria.
Alisema Tanzania inahitaji mbinu na mipango kazi ya kufikia malengo ya melenia ya mwaka 2025 inayolenga kuwapatia Watanzania wengi nishati hiyo ya umeme.
"Ndugu wana habari Marekani ipo tayari kuwekeza katika nishati hii na tayari tumewakilisha kwa waziri wenu mipango na mbinu iliyoandaliwa na wataalamu kutoka nchini Marekani kwa lemgo la kusaidia kuliondoa tatizo hili kama si kulimaliza kabisa" alisema Bw. Lenhardt
Alisisitiza kuwa Tanzania ina vyanzo vingi vya umeme ambavyo vikitumika uzalishaji wa nishati hiyo utaongezeka.
Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, alisema huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwekeza katika vyanzo vyake vya umeme ili kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema mojawapo ya tatizo kubwa inalolikabili Shirika la TANESCO ni uchakavu wa miundombinu hii inayochangia upotevu wa nishati hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment