LONDON, England
TIMU inayokipiga Ligi Kuu England, Chelsea imeingia makubaliano na kampuni ya inayoshiriki mashindano ya mbio za langangala maarufu kama Formula One, Sauber kuanza kutumia nembo ya kigogo hicho cha soka kwenye magari yake kunzia wiki ijayo, ikiwa ni sehemu ya kuongeza pato la timu hiyo mbali na soka.
Shirika la Habri la Marekani (AP), liliripoti jana kwamba kwa mkataba huo itashuhudiwa wanafainali hao wa Klabu Bingwa Ulaya na Sauber wakibadilishana uzoefu katika tasnia ya michezo, kufungua vitega uchumi na hisa pamoja na soko na fursa za udhamini.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Chelsea, Ron Gourlay alisema jana kwamba kwa makubaliano hayo, itashuhudiwa ushirikiano baina ya timu hizo mbili kuimarika tofauti na ilivyokuwa awali.
Makubaliano hayo yataifanya kampuni hiyo ya Sauber, kutumia nembo za timu hiyo inayovaa jezi za bluu kwenye magari yake ambapo zitaanza kutumika katika mashindano yatakayofanyika hivi karibuni katika nchi za China na Bahrain.
No comments:
Post a Comment