Na Rashid Kazumba
KINYANG'ANYIRO cha kumsaka 'Malikia wa Ukonga', Redds Miss Ukonga 2012 kinatarajia kutimua vumbi Jumamosi5 katika Ukumbi wa Wenge Garden Ukonga, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa JnC Intertainment, ambayo ndiyo waandaaji wa mashindano hayo Chiku Chambuso, alisema Dar es Salaam jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na warembo wote wapo fiti kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho.
Alisema mwaka huu Ukonga imejipanga kuhakikisha inatoa Redd's Miss Tanzania kutokana na kuwa na wanyange wenye vigezo vya hali ya juu.
"Tunatarajia mwaka huu tutafanya vizuri kuanzia kanda hadi taifa, tunataka kumtoa Redd's Miss Tanzania ambaye tuna uhakika atafanya vyema katika michuano ya Miss World 2012," alisema.
Alisema katika mashindano hayo jumla ya washiri 15, wanatarajia kupanda jukwaani kujinadi mbele ya majaji watakaokuwa na jukumu la kuchagua walimbwenda wenye vigezo.
Chiku alisema mashindano hayo yanadhaminiwa na Redd's ambao ndiyo wadhamini wakuu, Kiota Jungle, Kitwe General Traders, Vimax Logistics Clearing & Fowarding, Mambya Insurance Company, Mamushka Pup & Catering, Times Fm, Hiltech Resoute na Wenge Garden Hall.
Mratibu huyo alisema licha ya warembo kupanda jukwaani, pia kutakuwa na burudani ya nguvu itakayovurumishwa na bendi ya Mapacha Watatu.
No comments:
Post a Comment