17 April 2012

Millya ahamia CHADEMA

*Adai CCM ni gari yenye pancha lukuki
*Nape: Alikuwa mzigo ndani ya chama
*Shigela: Amejivua gamba, bado wengine
                            
                  Bw.James Ole Millya
Na Pamela Mollel, Arusha
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoani Arusha, Bw. James Ole Mallya, kutangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Bw. Mallya alitangaza nia hiyo mjini Arusha jana katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Kibo Palace na kudai kuwa, CCM imepoteza imani kwa wananchi baada ya kukosa mvuto kama ilivyokuwa zamani.

Alisema kutokana na hali hiyo, hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo ameamua kupanda gari salma lenye kutoa matumaini mapya kwa Watanzania.

“Leo natangaza rasmi kuihama CCM na kuachia nyadhifa zote nilizokuwa nazo kuanzia Mkoa hadi Taifa, najiunga na chama chenye dhamira ya kuwakomboa Watanzania ambacho ni CHADEMA.

“Naomba kunukuu maneneo ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliwahi kusema kuwa, CCM sio mama yake na mimi sio mama yangu, najiunga CHADEMA ambacho ndicho chenye kuleta tumaini jipya Watanzania,” alisema Bw. Millya.

Aliongeza kuwa, nafasi alizoachia ni pamoja na ile ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

“Kabla sijachukua uamuzi wa kuhama CCM, nilijitahidi sana kurekebisha baadhi ya mambo ndani ya chama lakini nilipuuzwa hivyo nikaamua kubadili mwelekeo kwa manufaa ya Watanzania.

“Vijana wengi walioko ndani ya CCM wanaishi kwa matumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya au Mkoa ila mimi siwezi kuishi kwa matumaini,” alisema Bw. Mallya.

Alitoa wito kwa vijana wote wenye nia na mapenzi mema ya Tanzania, kumfuata CHADEMA ambako ndio kwenye ukombozi wa kweli na tumaini la maisha ya Watanzania.

Bw. Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mwaka 2008 hadi sasa alipotangza kujiuzulu, aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru.

Alisema ameamua kwa ridhaa yake kuondoka CCM na kuachia nafazi zote alizokuwa nazo kwa sababu ya ukombozi wa kweli.

Hivi karibuni, Bw. Millya alijitosa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM lakini jina lake liliondolewa.

Wakati Bw. Mallya akitangaza kuhama chama hicho, vijana mbalimbali ambao ni wanachama wa CCM mkoani hapa, hawakuamini walichokisikia wakionesha dalili za kumfuata.

Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake, Bw. Hamisi Bakari, alidai kusikitishwa na hatua iliyochukuliwa na Bw. Mallya kuhama CCM na kukifanya chama hicho kionekane hakifai hivyo kilichobaki ni wao kumfuata aliko.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, amempongeza Bw. Mallya kwa kuchukua uamuzi huo ambao umekisaidia chama hicho kwa sababu alishakuwa mzingo ndani ya chama.

Bw. Nnauye aliyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii (facebook),na kudai itakumbukwa kuwa, Bw. Mallya alikuwa afukuzwe kwenye chama kutokana na mambo aliyokuwa akifanya.

Alisema CCM ilimpa karipio ili apate muda wa kurekebisha tabia yake hivyo ameondoka akiwa na karipio hilo.

“Kajivua gamba, tunampongeza kwa kuitikia wito, kila la kheri aendako ni kijana ambaye bado ana mengi ya kujifunza,” alisema Bw. Nnauye katika facebook.

Wakati huo huo, Mwandishi Pendo Mtibuche, anaripoti kutoka mjini Dodoma kuwa, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Bw. Martine Shigela, kujiuzulu kwa Bw. Mallya na kutangaza kukihama chama hicho ni ukomavu wa kisiasa na utekelezaji wa maamuzi yaliyotolewa na NEC ya kujivua gamba.

Bw. Shigela aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, kuondoka kwa Bw. Mallya ndani ya CCM, kumepokelewa kawaida kwani NEC ilishatoa maamuzi kuwa viongozi wa chama hicho na wanachama, wajipime, kujitathimini na kujiondoa wenyewe.

Alisema kitendo kilichofanywa na Bw. Milya kimeonesha ukomavu katika kutekeleza maazimio ya NEC ya kujivua gamba kwa wanachama wake hivyo anastahili pongezi kwa hatua hiyo.  

Aliongeza kuwa, viongozi wengine ambao wanajiona ni mzigo kwa  kwa chama hicho, wanapaswa wajiondoe kama alivyofanya Bw. Mallya kwani dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM Ni mchakato kwani haikumtaja mtu bali kila mmoja kwa wakati wake anatakiwa kujitathimini mwenyewe.

Bw. Shigela alisema kujiuzulu kwa Bw. Mallya, kutaisaidia UVCCM mkoani Arusha kujipanga upya ili kuendeleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Alisema sababu alizotoa Bw. Mallya kuwa ndiyo zilizomfanya ajiunge CHADEMA, si za msingi bali amejiona ni mzigo ndani ya jumuiya hiyo.

14 comments:

  1. CCM acheni Vioja. Kama Millya ni gamba asemavyo Nape, basi chama hiki kitakuwa kimejaa Magamba zaidi ya maelfu na maelfu.

    Magamba yanayo zungumziwa na Mh. Nape ni yale ambayo yeye aliyoyataja kisha akashindwa kuyatoa na bado yapo. Waombeni msaada CDM wasaidie kuyaondoa haya magamba.

    Nape na Bw, Shigela achaaneni na hivi vigamba mnganganie MAGHAMBA PAPA ambayo yanalindwa na kuhifadhiwa na chama chenu. Mellya ni kifaa kitakachoitesa CCM. Alikwisha wateseni ya kutosha. Kama hangalikuwa kifaa kwenu,kwa nini hamkufukuza mkawa mnambembeleza?

    ReplyDelete
  2. Wananchi wanategemea uboreshaji wa maisha na maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla. kinachotakiwa ni kuwa na dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania . kuhamia chama kingine bila kuwa na dhamira hii ni upotoshaji na pengine kusiwe ni kujijengea umaarufu kusikuwa na tija.WATU WATEGEMEE NINI? TUNAJIULIZA HIVI MPKA MTU AKOSE NAFASI FULANI NDIYO AONE UAMUZI HUO LEO. TUJIKOSOE, TUJISAFISHE NA TUJIPIME!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Wengi wataihama CCM tunapoelekea uchaguzi 2015. Ni dhahiri sasa CCM haina tena mvuto kwa wananchi. Magamba hayavuliwi kwa kuwa CCM hamna hata mmoja aliye msafi wa kumnyoshea kidole mwenzake.

    ReplyDelete
  4. unajua hakuna mwanasiasa mkweli tanzania hii, huyu jamaa yeye alikuwa namba moja kuiandia chadema na sasa ameenda huko. kaa ukijua watu hawa wanataa nafasi na kujineemesha wenyewe

    ReplyDelete
  5. huyu ndiye gamba la mkoa wa arusha,wako wengine watafuata mda si mrefu,nje alikuwa gamba nadini alikuwa chadema,kwa hiyo mnafikhina umefika mwisho,kila la heri na chama cha ngumi,hiki utafanana nao,huna jinsi,ubunge wa africa mashariki si macho wala umbo kubwa kama lako dogo.ni kichwa ni vichwa ndiyo wamekwenda kuwakilisha watanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe baki ukiwalinda wezi wanaoiba na kuhujumu mali za Watanzania. Nadhani wewe labda umeambulia labda kanga au wali ndio maana unawatetea. Amka! utetee wananchi. Hata ukiwa ndani ya CCM tetea wananchi. Linda mali za nchi ili sote tuboreke.

      Soma ripoti ya CAG uone jinsi serikali ya CCM inavyotafuna na wanaendelea kutafuna mabilioni ya fedha za wananchi.

      Akiwa UVCCM, Millya alikuwa anapiga kelele kutetea sio tu kwa ajili ya haki zake binafsi ila za wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla. Ametoka CCM ili aweze kuwatetea wananchi. Ukiwa ndani huwezi kuwatetea kwa kuwa CCM kumejaa magamba kama viongozi wao walivyotamka. "Toka nje ili ulithibiti jambazi lililokuvamia ndani ya nyumba hata kwa kupiga yowe. Ukiwa ndani litakuzidi nguvu.

      Vijana wengi wa CCM wanaogapa kukikosoa chama chao kwa hofu ya kupoteza kula yao hata kama wanatupiwa mifupa iliyomshinda fisi.

      CCM nako kuna waliohama kutoka vyama vingine na kuja kwenye chama hicho cha kulinda MFISADI. Hawa ni kama akina Guninita, Hiza Tambwe, Kabarou n.k Mbona hamuwaiti MAGAMBA?

      Delete
  6. CCM wakubali wasikubali kwa hili la Millya wametikiswa.Ni mfano wa KANU ilivyoanguka.Pamoja na hilo ni vizuri CHADEMA wakachukua tahadhali kabla au baada ya kumpokea mtu yeyote anayetoka CCM, ni vizuri wampime kwanza kama kweli amekuja kuungana nanyi kupigania haki za wanyonge au amekuja kutafuta madaraka? CHADEMA msisahau kilichotokea baada ya kumpokea Mhe.Shibuda baada ya kuupata ubunge mnajua alivyowageuka bungeni.

    ReplyDelete
  7. Mmmh ukiona comment za watu wengine utashangaaa.Ni hivi Mallya namfahamu sna kwa kauli zake pamoja na misimamo yake na nilijua huko hatakaa maana hawapendi watu wenye misimamo na mikakati ya kuwatumikia watanzania.Niseme tu bila kuficha hili linawatesa CCM sana,Mallya hakuwa Gamba na kama watu hamjui Nape MWENYEWE kashachoka na CCM isiyofufuka!, haieleweki yaelekea wapi? kila kukichwa ufisadi CAG mwenyewe kachoka kuandika hati chafu,Jamani nadhani walio kinyume na mtizamo wangu siwezi walazimisha na najua hawalipi kodi ndio maana hawanauchungu na nchi hii,tuamke nchi itafilisika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu wa hapo juu (saa 03.57)

      Nakuunga mkono ila kwa taarifa yako: HAKUNA RAIA AU MGENI ANAYEINGIA TZ, AMBAYE HALIPI KODI. MTOTO MDOGO AKINUNULIWA NEPI ANALIPA KODI. MZEE AKINUNUA KIBERITI ANALIPA KODI. MGENI AKINUNUA BIA ANALIPA KODI.

      TATIZO NI WANAOKWEPA KODI, WEZI WA MALI ZILIZOZALISHWA KWA KUTUMIA KODI ZA WANANCHI, MAFISADI,N.K.

      Ndio maana MAFISADI watalaaniwa milele na Watoto,Vijana wa shule na vyuo,mama wajawazito, walemavu, vikongwe, wagonjwa n.k kwa kuwa KODI wanazolipa zinatafunwa na haya MAFISADI (Soma ripoti ya CAG)

      Delete
  8. siasa za bongo BWANA! wananchi tuwe makini, huyu bwana alivyokuwa anapambana na kuifitinia CHADEMA, hata sipati picha!

    ReplyDelete
  9. naunga mkono hoja hii hapa juu umakini unahitajika hata shetani anasura nyingi sana anaweza kuja kama malaika wa nuru kumbe pepo kuweni makini na Mallya na CCM MSIPONDE HAYO NI MATUNDA YA UGHAID WENU MMEZIDI KUFIRISI NCHI UKWELI MNAO WENYEWE ONDOENI VIBANZI NDANI YA MACHO YENU NDIPO MTATOA BORITI NDANI YA JICHO LA Mallya hizo ni ngome ambazo zinatikisika bado kuanguka ukuta watanzania tunaunga mkono maamuzi yake lakini asiwe kigeugeu na kama ametumwa aondoke kabla hajaondolewa.

    ReplyDelete
  10. hapo zamani za kale palikuwa na sungura aliyetafuta chakula alipofika katika shamba aliona mgomba wenye mkungu wa ndizi mbivu zikitamanisha alipojaribu kurukia hakufanikiwa alipoona ameshindwa akasema sizitaki mbichi hizi, naona nafanya kazi bila faida kujua ccem poleni hamzitaki mbichi wakati zimeiva teh tehe tehe!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. wana ccm wanamtindio wa hakili wakili udhaifu mbona wanazidi kuhama wengi je,na hao watasemwa je, na wana ccm wajue kuwahama pia nikujivua gamba kwani wanao nga'ngania ccm wanamagamba kwani wanachama wote wa ccm wanayo by SEMAGOGWA ELIUD ZAWAD (KIGOMA)

      Delete
  11. tupambane kwa pamoja 2015 ni CHADEMA na mimi ntapambana na mubunge wa BUYUNGU-KIBONDO BY SEMAGOGWA

    ReplyDelete