24 April 2012

Maskini Lulu, amwaga chozi mahakamani

Na Rehema Mohamed
MSANII maarufu wa filamu nchini Elizabert Michael 'Lulu' jana alimwaga chozi Mahakamani wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msanii huyo alimwaga chozi hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na msukumano kati ya askali magereza na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwa wakitaka kumpiga picha.

Waapigapicha hao walikuwa wanampiga picha Lulu wakati akitokea katika gari la magereza aliloletwa nalo na kupandishwa mahakamani ambapo askali magereza waliweka ulinzi mkali uliofanya wapigapicha wasipate nafasi nzuri ya kufanya kazi yao.

Hali hiyo ilileta tafrani na msukumano mkubwa na kumfanya Lulu aliyekuwa akisindikizwa na askali wa kike zaidi ya watano kuwa katika wakati mgumu ambapo hadi anafika kizimbani alionekana akitokwa na machozi.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo,wakili wa serikali Elizabert Kaganda,mbele ya Hakimu Lita Tarimo aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

Kutokana na hali hiyo aliiomba mahakama hiyo itowe tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa ambayo ni Mei 7 mwaka huu.

Kaganda baada ya hakimu kutoa tarehe hiyo,aliiomba mahakam hiyo itoe amri ya watu waliokuwa katika kordo za mahakam hiyo kupungua ili mshtakiwa huyo atoke kwa usalama.

"Mheshimiwa hakimu naomba mahakama yako itoe ami ya watu kupungua ili mshtakiwa aweze kupita kwa ulinzi na usalama kwasababu ameingia ka kusukumwa sukumwa kutokana na watu kuwa wengi"alidai Kaganda.

Tarimo hakuwa na pingamizi na ombi hilo na kuwaamuru maaskali walio mahakamani hapo kuondoioa watu wote wasiohusika ili mshtakiwa apite kwa ulinzi na usalama.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi katika akiwa ndani ya basi dogo la kijani la magereza kaiwa mshtakiwa pekee katika basi hilo pamoja na maaskali magereza.

Katika msafara huo,Lulu alisindikizwa na magari matatu likiwemo aina ya civilian STK 3058 lililokuwa limejaa askali wa kutuliza ghasia waliokuwa wakiwa na virungu pamoja na ngao.

Lulu anatetewa na mawakili watatu ambao ni Peter Kibatala,Keneld Fungamtama,Fulges Masawe na Kamishna wa Haki za Binadamu.

35 comments:

  1. Kwako Muandishi wa habari hii..

    Inasikitisha na kutia kichefuchefu pale unaposhindwa hata kutumia maandishi ya kiswahili kwa usahihi, badala ya askari - unaandika askali, amri - unaandika ami, kuondoka - unaandika kuondoioa, sasa hiyo ni haraka au ni kukosa umakini wa kukagua kazi yako kabla ya kuichapisha? Je mhariri wa gazeti uko wapi?

    Usiwe mvivu wa kukagua kazi yako, mwisho wa siku ni muonekano wako wewe kama wewe pia Kiswahili ni lugha yetu ADHIMU ni lazima tuitumie kwa ufasaha - au ndio ule usemi usemao -
    1. Kuna watu wanakwenda kazini
    2. Na kuna watu wanakwenda kazini kufanya kazi
    Sasa na wewe jichunguze kwa makini je uko kwenye kundi lipi? - la wanaokwenda kazini au wanaokwenda kazini kufanya kazi?

    Rochas
    Zanzibar

    ReplyDelete
    Replies
    1. usimwonee bure, waandishi wetu wa kiswahili (kibongo) hawana facilities za kisasa, hivyo huchukua story kutoka eneo la tukio kwa peni ktk notebook na kuipeleka kwa typist ipigwe ikesha mhariri ndio ana-i-approve! sasa hilo tatizo dogo la typographical error lisikufanye ukam-downgrade mwandishi na profession yake bure kwa kosa la typist! Mhariri ame-oversee it, ana kazi nyingi, tumuelewe! wacha criticism zako zisiompango! zinalenga kuvunja muungano kwa kudai waswahili safi ni wa ki-zanzibari na wanyamwezi hawajui kiswahili!

      Delete
    2. unaposema mwandishi kakosea kuandika unakosea. kwa sababu sio lazima mwandishi awe ndio MCHAPAJI. fikiria kabla hujalaumu.

      Delete
    3. Mchapaji anachapa alichopelekewa sio kazi yake kuangalia lugha kumbuka gabbage in...gabbage out!

      Delete
  2. Jamani acheni kuhusisha mambo ya Muungano na usahihi wa lugha ya kiswahili. Nani kasema kuwa kiswahili sahihi kiko Zanziba tu.
    Tuelewe kuwa ndugu Rochus alikuwa anatoa maoni yake tu basi na wala hajasema eti watu wa bara hawajui kiswahili

    JAMES MBELE
    SHINYANGA

    ReplyDelete
  3. hivi kuna mtu asiye kosea?kama wewe unaye kosoa wengine chukua muda wako jichunguza mambo ya fuatayo tabia yako,jinsi ulivyo mwenyewe je upo sawa na ulivyo?akili hufikili uwezo wako elimisha na siyo kukosoa.hakuna mtalaam wa lugha wala mzawa wa lugha au mwenye lugha wote tyunajifunza baada ya uikuta.Tena yaonekana ROCHAS hujui zaidi ya aliyeosea mtanzania wa kweli huelimisha si mtukanaji Valentine Nairobi kenya

    ReplyDelete
  4. Waandishi kuweni makini na kazi zenu,hasa errors kagua kazi kwanza kabla ya kuichapa.

    ReplyDelete
  5. Kulaumu mimi nadhani sio kitu kibaya hasa kwa kazi yenye makosa mengi kama hiyo anapaswa kulaumiwa na ni lazima awe makini na kazi yake.Valentine wewe mwenyewe una makosa mengi hebu isome hiyo koment yako uangalie.Na kuhusu kiswahili kizuri kuwepo Zanzibar hilo lipo wazi kabisa kwani hata historia inaonyesha hivyo.

    ABDALLA ABEID

    ReplyDelete
  6. lazima mtu akosolewe ili kuweza kujifunza tuna nia ya kubwa ya kukuza kiswahili na vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika hili wacha hakosoe ili kujenga kiswahili kizuri na fasaha kitakachotutambulisha kwamba hii ndo lugha yetu na chimbuko lake ni Tanzania tunakosoana ili tujifunze na asiye kubali kukosolewa sio msomi.

    ReplyDelete
  7. Huyo mwandishi lazima alaumiwe kwa makosa aliyofanya ili ajirekebishe,pia Mhariri wa hiyo habari anastahili kukosolewa pamoja na mfumo mzima wa kudahili wanafunzi katika vyuo vya uandishi wa habari kwa kuchukua Vihiyo.Unapokuwa Mwandishi au Mtangazaji inabidi lafudhi na kasoro za lugha ya kikabila uiache na uendane na matamshi sahihi ya lugha husika inayotumika katika taifa lako yaani Received Pronunciation.

    ReplyDelete
  8. This is too much of prostitution news.We need development stories you journalists.

    ReplyDelete
  9. Tanzanians need to know when poverty will end as well as the longevity of financial fluctuation and not love news.

    ReplyDelete
  10. Tanzanians need to know when poverty will end as well as the longevity of financial fluctuation and not love news.

    ReplyDelete
  11. Tanzanians need to know when poverty will end as well as the longevity of financial fluctuation and not love news.

    ReplyDelete
  12. nafikiri kuna watanganyika wengi wanaumwa kuiona zanzibar au wazanzibari wanadai haki yao kutoka kwa mkoloni mweusi- tanganyika.

    Maana haiwi mtoa maoni amemkosoa muandishi na Kiswahili chake Kibovu... Anakuja Huyu Punguani kutaja muungano na zanzibar.. inahusu nini? hebu jibu Hoja dada wee. acha ujinga na chuki juu ya wazanzibari

    ReplyDelete
  13. Nadhani wote wanaolaumu mwandishi huyu hawaelewi lengo kuu la mpashaji habari. Kama ujumbe uliokusudiwa umefikishwa basi kazi inakuwa imefanyika 100%. Achilia mbali makosa ya lugha, ujumbe uliokusudiwa umetufikia na tumeelewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari ni muhimu iandikwe kwa lugha fasaha...kuendekeza ubabaishaji si sawa! Tuache kutetea uozo katika taaluma ya upashaji habari.

      Delete
  14. Nadhani wote wanaolaumu mwandishi huyu hawaelewi lengo kuu la mpashaji habari. Kama ujumbe uliokusudiwa umefikishwa basi kazi inakuwa imefanyika 100%. Achilia mbali makosa ya lugha, ujumbe uliokusudiwa umetufikia na tumeelewa.

    ReplyDelete
  15. Au anatafuta nafasi ya kazi ambayo mwenzie anaifanya? Mbona lawama nyingi sana?

    ReplyDelete
  16. cha muhimu habari imeeleweka kosoro za kilugha kila mtu anazo kutokana na lugha ya mama au mazingira aliyokulia mchapaji. Kijitenga kwa Zanzibar ni suala lingine wala halihusiani na hili.

    ReplyDelete
  17. nampa pole sana dada(lulu),inavyoonyesha inaelekea kula kwake.hii ni kwasababu ya vithibitisho vilivyofikishwa mahakamani vinavyoonyesha kuwa ana umri zaidi ya miaka 18.ni pamoja na Passport na video clip aliyojieleza mwenyewe kuwa amesha timiza umri wa miaka 18+

    ReplyDelete
  18. alafu na huyo Mdee na mwenzaake,kinacho wagusa hasa na kuwakera nn!?wafanye vitu vilivyo wapeleka bungeni.nchi inawashinda.hebu waendeleee na Budget!

    ReplyDelete
  19. unayesema ni kutafuta kazi ambayo mwenzako anaifanya cyo kweli kwani wanakuwa na makosa mengi sana katika uchapishaji kwa kweli wajirekebishe, na kazi ikipelekwa kwa typist inabidi uliyepeleka ukaifanyie editing na cyo uwe mvivu wa kuipitia kuna makosa yanayoweza kujitokeza madogo madogo lakini cyo kila ukisoma mstari mmoja kosa, wa pili kosa huo ni kutokuwa makini na kazi yako, chezea mshahara na cyo kazi.

    ReplyDelete
  20. hakikisha unapolish your work.....twende kazini kufanya kazi...sio twende kazini kutia siku...

    ReplyDelete
  21. tumsamehe jamani alikuwa amechoka kila mtu anachoka au sio?

    ReplyDelete
  22. hiv mlilazmishwa kucomment mbn mnamlaumu mwandishi badala ya kucomment yanayowahusu ictoshe c lazma km hujickii acha alaa!!

    ReplyDelete
  23. Tuache kukosoana zaidi tutoe maoni ya kumkomboa Mtanzania katika masuala ya kiuchumi,kijamii,kisiasa,kiutamaduni katika wakati huu wa utandawazi between(Globalizers and Globalized).

    ReplyDelete
  24. pole mrembo, huo ndio ukubwa. hata kama ikigundulika huna hatia katika kifo cha huyo anayedaiwa alikuwa mtu wako, hamna shida utakuwa umejifunza kuwa makini katika maisha yako, kwani maisha ukiyachezea yanakunyonga. ujifunze uwe mtu mzima sasa, unasikia? mambo ya uchangu uache sasa, wewe ni mrembo wa kutosha tulia uolewe ndoa ya heshima huku ukipiga kazi yako ya usanii

    ReplyDelete
  25. Mtu anayeposti ukurasa huu kwenye website ni Kihiyo wa hatari kutoa anaandika kuoa, kweli mtu anaweza kuoa matamshi au kutoa matamshi. Wekeni watu makini kuna watanzania wazuri wamejaa mtaani wanaoweza kufanya kazi vizuri, hii inaweza kuwa matokeo ya kupeana kazi kiukoo.

    ReplyDelete
  26. mabinti acheni mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo kwani mnaweza kupata matatizo kama ya mwenzenu.Wazazi tukae na watoto wetu tuwaelimishe kuhusu madhara ya mahusiano katika umri mdogo waelekezwe mila na desturi zinazohusu mahusiano ya kimapenzi(African perspectives on sexuality).Hii itasaidia kuwaandaa vijana kuepukana na matatizo kama ya LULU pia vijana wa kike na kiume wakisaidiwa na viongozi wa dini kwamba ni wakati gani wanatakiwa kuanza mahusiano ili kukubiliana na upepo wa kimagharibi unaoathiri kizazi cha sasa.

    ReplyDelete
  27. Kazi ya muandishi haitoshi kutoa habari tu, ni kuhakikisha habari ameitoa kiuhakika, kimaana na kimaandishi, je mtu akiielewa habari kinyume, litakuwa kosa la nani?.(mwandishi), dereva wa gari sio kuendesha tu, bali kwa usalama.

    ReplyDelete
  28. hivi ni wakati gani tutatambua kuwa hatuhitaji kutokea kwa kosa kwanza ndiyo tupate fursa yakujifunza ama tuweze kuelimika. kujifunza kunakuwepo tu licha ya kuwepo kwa makosa. mwandishi wa habari hii ni dhahili hakuwa makini katika uandishi na uhariri wake. lakini pia hatuwezi kuhalalisha makosa haya katika misingi na mitazamo kuwa kila binadamu hukosea, dhana hii ina ni nzuri lakini si sahihi sana kila kulikinga na ubinadamu. makosa ya kazi hii ni mengi mno.

    ReplyDelete
  29. Sio siri; Majira wamezidi kuandika vitu vya ajabu. Kukosea ni kitu cha kawaida lakini inapozidi inatia kichefuchefu. Kama tatizo ni mchapaji kashindwa kazi basi watafute mwingine. Tatizo watanzania sasa hivi tunachakachua kila mahali. Waandishi wetu wamekuwa wa kuokotakota tu bila sifa. Ndiyo maana hata uchambuzi wa habri unawashinda maana kwao uandishi ni kuripoti tu. Lakini hata kama wameamua kubakia kuripoti basi waandike kwa usahihi.

    ReplyDelete
  30. Pole Lulu haikuwa tu bahati yako.

    ReplyDelete
  31. Sasa nyie izo Comment zimuhusu Lulu au Mchapishaji? Mbona mnakuwa na akili fupi kiasi hicho, ni makosa tu katika kuandika kama hamna Comment za maana nendeni mkalale.
    Huyu lulu anapaswa kutiwa adabu badala ya kusoma anaangaika na midume yenye wake zao. Huyo Lulu hana ujanja tena akimaliza kifungo chake tuone kama ataendelea na umalaya wake tena.

    ReplyDelete