12 April 2012

CHADEMA waweka mkazo Serikali za majimbo

Na Raphael Okello, Bunda
CHAMA cha Demokrasia na Mae n d e l e o (CHADEMA) kimesisitiza kuwepo kwa serikali ya majimbo ambapo kimewaomba wananchi kuzingatia suala hilo watakapotoa maoni wakati wa mchakato wa uandikaji wa Katiba Mpya.

Akiwahutubia mamia ya wananchi mjini
Bunda mkoani Mara hivi karibuni Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana Bw. Ezekiel Wenje
aliwataka Watanzania kuingiza katika Katiba
Mpya ijayo utawala wa majimbo kwa kuwa
ndio njia pekee itakayowawezesha wananchi
kufaidi uwepo wa rasilimali ya nchi.
"Hatuwezi kufaidi rasilimali ya nchi kama
mfuko wa taifa utaendelea kuwa mmoja...kwa
kuwa wapo viongozi wajanja wanaotumia
vibaya mgao huo ambapo fedha nyingi
huishia katika mfuko wao huku wananchi
wakitaabika," alisema Bw. Wenje.
Alisema zipo kanda ambazo zina rasilimali
nyingi lakini hazina maendeleo ambapo alitoa
mfano kwa Kanda ya Ziwa ambapo alisema
kanda hiyo inamiliki rasilimali nyingi ya taifa
ikiwa ni pamoja na rasilimali watu, madini,
ziwa, wanyamapori, samaki na zao la pamba
lakini kanda hiyo bado iko nyuma katika
huduma za jamii na kwamba haina hata Chuo
Kikuu kimoja cha Serikali.
Aliwataka wakazi wa Kanda ya Ziwa na
kanda zingine kuhakikisha kuwa ajenda hiyo
inakuwa ni ya kikatiba na si ya chama cha
siasa kwa kuwa inagusa utaifa.
"Idadi ya Watanzania inakadiriwa kufikia
milioni 45 na kati ya hao milioni 15 wanatoka
kanda ya ziwa...na katika nchi hii mgombea
yeyote wa kiti cha urais lazima atafute kupata
ukubali kutoka Kanda ya Ziwa ili apate
uhakika wa kushinda," alisema Bw. Wenje.
Kwa mjibu wa Bw. Wenje kupitia mgawanyo
wa mapato ya rasilimali katika serikali ya
majimbo ni asilimia 20 ya mapato yote ndio
itakayowasilishwa katika mfuko wa pamoja
wa taifa ili kufidia majimbo yenye rasilimali
kidogo na shughuli za jumla za umoja wa

2 comments:

  1. Ndugu zangu tunapohubiri sera za majimbo tufahamu fika tunahubiri kuligawa TAIFA. Sera hiyo si makini na ni HATARI kwa UMOJA WETU, UDUGU WETU, AMANI YETU NA UTAIFA WETU.

    Amani Millanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba chama cha Demokrasia na Maendeleo kifanye jitihada za haraka kueleza na kufafanua kwa upana dhana hii ya majimbo.

      Tusihusishe Sera ya Majimbo na makabila. Mwalimu alikwisha ondoa balaa hili la ukabila. Makabila yote yamechanganyika na yamesambaa nchi nzima kuanzia Mmasai hadi Myao n.k. Tuzungumzie Sera hii kuimanisha SERA YA MAENEO bila kujali kabila lipi liko maeneo hayo. Tuachane na wenye dhana hii potofu ya ukabila kwa manufaa ya KISIASA. Kupendana bila chuki kwa Watanzania kupo na kumekomaa.

      CHADEMA nawashauri mtafuteni katiba za nchi mabali mbali zenye mfumo huu. Chapisheni nakala za baadhi ya katiba hizi mkiangazia vipengele ambavyoo vitaifaa Tanzania. WATANZANIA hawawezi kuchangia mada ambayo hawajaeleweshwa vizuri.Tumieni Wataalam wa Vyuo Vikuu na vyuo vyote kama Maprofesa, wanafunzi, wananchi n.k ili kupata nakala za katiba hizi na kuzieneza kwa Watanzania kupitia vyombo vya habari k.m radio, TV, magazeti, internet, mikutanoni n.k.Lazima kuwe na Reference ya kuanzia na kulinganisha.

      Hata tume yetu ya kutayarisha Katiba yetu mpya itatumia reference hizi. Waombeni wawape nakala. Ni kazi ya TUME kutoa mafunzo na sio kuficha hii mifano ya katiba za nchi nyingine.

      Tukiangazia mfano wa SERA ya majimbo, ueleweshwa huu utamtoa wasiwasi ndugu yetu hapo juu na WATANZANIA kuhusu hisia yake potofu kuwa ikiwa SERA ya majimbo itatumika, inaweza kuligawa TAIFA.

      UGAWAJI NA USIMAMIAJI MZURI WA RASLIMALI ZETU KWA USAWA NDIO UTALETA AMANI YA KWELI.
      HAKUNA SABABU YA MIKOA MINGI KUWA MASKINI NA MINGINE NI TAJIRI.

      Sana sana, MTINDO Wa bajeti wa sasa ulivyo unaligawa TAIFA Kimaendeleo. Katika Bajeti nyingi za Serikali yetu hazigawi fedha kwa uwiano kuzingatia hali halisi ya kimaendeleo kwenye mikoa na wilaya. Mikoa iliyo pembezoni au katikati ya nchi ambayo haina raslimali na vyanzo vya asili vya mapato ingebidi WAPEWE FEDHA ZAIDI KUTOKA kwenye bajeti ili wafanane na ile mikoa yenye raslimali nyingi kama madini, misitu, mvua za kutosha, vivutio mbali mbali vya watalii.

      Kwa mfano, Mwanza inabidi ikazane na ichacharike kutumia na kutunza hizo raslimali walizonazo kibiashara ili Serikali iweze kupata kodi zaidi ambapo fedha hizo za kodi zitaelekezwa kwa mikoa isiyo na raslimali.

      Kieleweke kuwa raslimali zote ni za Watanzania wote. Tusibaki kuwasakama wananchi wa Mikoa iliyo na uchumi duni kuwa ni wavivu,hawana miundo mbinu mizuri ya kufikisha mazao yao sokoni, Wabunge wao hawana influence bungeni n.k.

      Siimanishi kuwa Mikoa yenye raslimali nyingi itakuwa inatoa fedha kama sadaka au misaada kama tupatayo kutoka nchi za nje. Ni wajibu wao kwa kuwa kodi ni ya lazima na haitolewi kwa hiari. Hii itaifanya Mikoa isiyo na raslimali isijione kama ombaomba. Itakuwa ni haki yao.

      Delete