*Kauli za wagombea zachochea uvamizi wa shamba
*Wananchi waharibu mali, nyumba za wawekezaji
*Wadai kuambiwa mashamba hayo ni mali yao
Na Queen Lema, Meru
ZAIDI ya wakazi 300 waishio Kata za Maji ya Chai na Maroroni, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, juzi walivamia shamba la mwekezaji zaidi ya ekari 6,000 lijulikanlo kama Doll Estate.
Mbali ya uvamizi huo, wakazi hao waliwavua nguo zote walinzi wa shamba hilo, kuharibu mali na kuiba vifaa mbalimbali.
Akizungumza na Majira jana, Msimamizi wa Idara ya Wanyama katika shamba hilo, Bw. Robson Peter, alisema wakazi hao walifanya uvamizi huo saa 11 jioni.
Alisema wakazi hao walidai kuwa, shamba hilo ni mali yao kama walivyoambiwa na baadhi ya wagombea ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki.
“Wananchi waliovamia shamba hili ambalo linahusika na ufugaji wa wanyama mbalimbali kama twiga, swala, pundamilia na wengine walikuwa na silaha za jadi wakidai kuwa, hawataki kuona wawekezaji wa kizungu ndani ya shamba hili,” alisema.
Bw. Peter alisema baada ya wananchi hao kuingia ndani ya shamba wakiwa wamevunja ukuta wenye urefu wa zaidi ya kilomita nne, waliwakamata walinzi, kuwavua nguo zote na kuwapa adhabu huku wengine wakiendelea kufanya uharifu wa mali katika nyumba za wawekezaji.
Alisema kutokana na uvamizi huo, walilazimika kutoa taarifa Kituo ch Polisi Meru ambacho kilituma askari ambao ndio waliofanya kazi ya kuwatawanya wavamizi hao kwa mabomu ya machozi.
Awali baadhi ya wawekezaji katika shamba hilo ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema kilichofanywa na wananchi waliofanya uvamizi huo hasa kutoka Kijiji cha Kitefu si
cha uungwana kwani walikuwa wakiishi kwa ushirikiano mkubwa.
“Sisi tupo katika shamba hili kwa mujibu wa sheria, tunashangaa wakazi wa kata hizi kusema hawataki kutuona wakati sisi tuna haki, leo hii wamevunja nyumba zetu na kuchukua mali, hatujapendezwa na hali hii hata kidogo,” walisema wawekezaji hao.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa kata hizo walisema kuwa, kuvamiwa kwa wawekezaji hao kunatokaa na kauli za siasa zilizotolewa na viongozi mbalimbali kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo.
“Juzi viongozi wa vyama viwili ambavyo vilikuwa vinachuana
walidai haya mashamba ni mali ya wananchi ambao waliamua kwenda kufanya uvamizi ili kuchukua shamba hili, nguvu ya ziada inahitajika ili kukomesha tabia hii,” walisema.
Diwani wa kata ya Maji ya Chai Bw. Loti Nnko, naye alijionea uharibifu wa mali za wawekezaji na kudai hadi sasa, thamani halisi ya uharibifu huo haijajulikana.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye, amethibitisha kuwepo tukio hilo na kudai jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi zaidi.
Lindeni wawekezeji waliopo kihalali, kwavile wako watanzania ambao wamewekeza nje ya nchi pia. Hatutafurahi ksikia wamevamiwa na kunyang'anywa mali zao. Wawekezaji wajanja washughulikiwe kisheria, warudishe mali ya wananchi bila fujo.
ReplyDeleteJe!Uhali ni upi? Serikali iangalie upya suala la ardhi za Meru zilizoko mikononi mwa wageni.
DeleteNinavyojua mimi hii ni mvua ya rasharasha, masika bado! Waliouziwa ardhi ya wananchi kwa kigezo cha uwekezaji wanapaswa kuzibua masikio na kufungua macho! Huko kwao wanaweza kumwuzia mwafrika ardhi ili wafuge nyani na tumbili? hata kama walipata ardhi hiyo kwa mujibu wa sheria, wajue maandishi yameshawekwa ukutani! Wachukue kilicho kwao na kutokomea walikotoka. Ya Zimbabwe yaja!
ReplyDeleteYaani hii nchi imeuzwa kabisaaa. Huwezi kuniambia kazi hata ya upishi watanzania hawazezi...Wazungu wameshatuzidi maarifa. Hilo shamba la katani liliwazesha watu kupata ajira na pia kujipatia chakula cha mifugo. Sasa ajira hawana na pia wamefungiwa hadi njia za kupita. Wazungu wanawaona wananchi kama nyani tu...acha waonyeshwe.
ReplyDeleteMabomu kila mahali hadi lini? Shamba hili la Dolly Sisal Estate ni mali ya mwekezaji yupi? Inavyoelekea mchukuaji mmoja amewaleta wenzake kibao? Na kama wao ni wachukuaji wa kisheria kwa nini hawataki majina yao yaandikwe au kutajwa? Maoni yangu ni kuwa haya ni yale yale ya mmiliki wa Dowans na Kagoda ambapo mimi sijawafahamu hadi leo. Sheria na mambo ya lease yatazamwe upya badala ya kupiga watu mabomu. Uchunguzi uwe zaidi ya mali za hao wafuga twiga kuharibiwa mali zao.Viongozi wa vyama vipi waliosema hilo ni shamba la wananchi? Vyama hivyo viwekwe bayana ili ajulikane mkweli ni nani? Tuwe wazi
ReplyDeletewamewekeza nini katika hilo shambala twiga?
ReplyDeleteKwa maoni yangu uvamizi ndiyo njia pekee itakayoifanya serikali yetu kiziwi kusikia maumivu ya wananchi. Hili likishindwa, hatua itakayofuata ni kuwaua mbwa wanaowalinda hawa wavamizi wa kigeni na hilo likishindwa tuwashughulikie wao. Iweje wazawa walale na njaa na kiu kwa sababu ardhi na mito yao imehodhiwa na wakimbizi wa kigeni halafu sisi tukae kimya? Serikali ya CCM iko likizo tuizindue kwa kuwafinya hawa marafiki zao waliotuletea kifisadi. Maumau waliwacharanga wazungu mapanga wakafaulu kuikomboa ardhi yao. Mapanga tunayo, mishale na mikuki pia. Tutetee ardhi yetu.
ReplyDeleteSheria izingatiwe wakati wa kufanya maamuzi fulani, kama ni kuwaondoa hao jamaa itumike sharia na sio nguvu kubwa namna hiyo. Fine wanaweza kuwa hawana haki kumiliki mashamba hayo, je mwanzoni yalikuwa yanamilikiwa na nani? je yaliendelezwa? Nani aliwauzia hilo shamba, hao wanyama wanawafuga kihalali au ndo wale wakupandishwa ndege?
ReplyDelete