30 March 2012

Zitto atetea msimamo wa POAC

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), Bw. Zitto Kabwe, ametetea uamuzi wa kamati yake wa kutaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) anyang’anywe jenereta na kwamba hatua hiyo itamsaidia kujua kuwa umeme umekatika.

Akijibu maoni ya watu mbalimbali
kupitia mtandao wa Mabadiliko jana,
Bw. Zitto alisema; “ Shirika linalopaswa
kuhakikisha umeme unapatikana muda
wote, Bosi wake anapewa stahili ya
jenereta umeme ukikatika.”
Alisema, TANESCO lina jukumu
la kuhakikisha nishati ya umeme
inapatikana kwa wananchi wote.
“Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO
ndiye Mtanzania aliyepewa jukumu
hilo na Taifa. Iwapo mkurugenzi mkuu
wa TANESCO anawekewa stahili
katika mkataba wake kwamba ‘atapewa
standby generator itakayolipiwa na
Shirika’ maana yake ni kwamba mgawo
au kukatikakatika kwa umeme ni jambo
litakalokuwepo tu,” alisema.
Alisisitiza kuwa jambo hilo ni
dogo lakini lina maana kubwa, hivyo
Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO
haikupaswa kuweka stahili hiyo.
Alisema kimsingi, waziri wa nishati
hapaswi kuwa na jenereta nyumbani
kwake, iwe ya kulipiwa na Serikali au
ya kujilipia mwenyewe.
Kuhusiana na TANESCO kutopewa
fedha alisema kamati imekuwa kali
sana kwa serikali. “Kamati ilimwita
Katibu Mkuu kuhusu suala hilo. Kamati
imeagiza kwamba suala hilo limalizwe
haraka iwezekanavyo,” alisema.
Alisema, POAC inajitahidi
kuhakikisha mashirika ya umma
yanatimiza wajibu wake

4 comments:

  1. Mh. ZITTO NA KAMATI YENU, FANYENI KAZI ZENU MLIZOTUMWA NYIE SIO WATENDAJI AU MAJAJI KATA. TANESCO AU MASHIRIKA YA UMMA YANAFANYA KAZI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU (REGULATIONS) ZAKE.

    TANESCO INA BODI YAKE, INA WIZARA MAMA, INA SERIKALI KUU. JE, KAMA HUYO MKURUGENZI AMEPEWA RUHUSA ATUMIE HILO GENERATA NA BOARD YAKE AU WAZIRI WAKE AU RAIS NYIE MNATOKA WAPI NA HAYO MAAGIZO?

    HAPA HAKUNA MAMBO YA KUTUMIA MISULI. MLICHOTAKIWA KUFANYA NI KUWAJULISHA VIONGOZI WAKE WA JUU WACHUKUE HATUA. WALA MSIMWAGIZE MKUU WAKE ACHULUE HATUA GANI. ONA WEWE NA KAMATI YAKO MNAVYOAIBIKA! HAPA SIO MAMBO YA SIASA. HATA WAKUBWA WAO WANANYAMAZA KIMYA NA WANAWACHEKA. AMEGHAIRI, WEWE UTACHUKUA HATUA GANI NA HUKU UMESHAWARUKA WAKUBWA WAKE?

    AU MNATAKA KUMKATISHA TAMAA HUYU MKURUGENZI ILI AACHIE NGAZI NA NYIE MTEUE MNAYEMPENDA? HAPA UTETEZI UMMA HAUSAIDII. ANGALIA,JIFUNZE SAYANSI YA UENDESHAJI WA SERIKALI. WEWE NI KIJANA NA UNAWEZA KUJIFUNZA HARAKA. KAMA WANANCHI WATAKUPA URAIS UNAVYO TARAJIA WAFANYAKAZI NA WANANCHI KWA UJUMLA WATAPONA? BUSARA ITUMIKE!

    KAZI ULIYOPEWA NI YA KUKUJARIBU UELEWA WAKO WA MAMBO. UTUMIE WAKATI HUU VIZURI. TUTAKUSOMA ZAIDI.....

    ReplyDelete
  2. Ndiyo maana hawa wadudu wabaya kwa sera za kulindana yaani wakurugenzi wanakaa na kutoa maamuzi kama haya “ Shirika linalopaswa
    kuhakikisha umeme unapatikana muda
    wote, Bosi wake anapewa stahili ya
    jenereta umeme ukikatika."

    ReplyDelete
  3. Weye ndugu uliyetoa maoni juu ya kazi ya POAC hUJUI KITU NA YAWEZEKANA WEWE NI NDGU YAKE NA MKURUGENZI AU MNAOCHANGIA NCHI KUIBIWA,MAANA UNASEMA USICHOKIJUA.WEWE UNAMTETEA MKURUGHENZI.HAJUI UMEME UNAVYOKATIKA.ETIMASHIRIKA YANAFUATA SHERIA,SHERIA GANI ZA KIJINGA NA KULINDANA HIZO.MTABAKI MIFUTA TU WATANZANIA KAMA HAMTAKUWA WAKALI NA NCHI YENU.KWA NINI APEWE JENERETA?? IKIWA KUNA MAANA KWAMBA UMEME KUKATIKA NI JADI YETU,HIVYO MKUBWA APEWE GENERETA.NADHANI NI MJOMBA WAKO.ACHA USHAMBA TAFUTA CHAKO,USIJIPENDEKEZE KWA MJOMBA.

    ReplyDelete
  4. Kwa wewe wa saa 2.53 AM. Ya ushamba tukuachie wewe. Soma pole pole na kwa utulivu uelewe nilichosema au urudi darasa la saba kwenye somo la INSHA ujifunze zaidi.

    Kwa kifipu nilichoandika ni hivi: POAC wangemwendea Mwenyekiti wa Bodi au Mkuu mwingine wa Mkurungezi. Wakuu wake ndio wangalimwambia arudishe Generata na sio POAC kutoa maagizo moja kwa moja kwa Mkurugenzi. POAC wasiiogope Bodi. Bodi na Wizara ndio size ya hawa Wabunge. Wapambane na hawa wakubwa. Mkurugenzi ni mtu mdogo sana kiutawala kwa POAC.

    Kama atakuwa ametenda kosa basi viongozi wake watamchukulia hatua pengine zaidi ya hilo agizo la POAC
    Sijamtetea Mkurugenzi popote ila utaratibu uliotumika. Hapa inatumika Sayansi ya uongozi na si siasa.

    ReplyDelete