Na John Gagarini, Pwani
WAKAZI 41 wa Kijiji
cha Pongwe wilayani
Bagamoyo Mkoa wa
Pwani wamelazwa hospitali baada
ya kula samaki wanaosadikiwa
kuwa na sumu.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa
Polisi mkoani humo jana Bw.
Ernest Mangu alisema tukio hilo
lilitokea Machi 29, mwaka huu
katika kijiji hicho kilichopo Kata
ya Msata ambapo mama mmoja
asiyefahamika aliwauzia wakazi
hao na kuwasababishia kuumwa
na kukimbizwa kwenye Kituo cha
Afya Msata.
Kamanda Mangu alisema, samaki
hao walikuwa wamekaangwa na
mama huyo na kuwauza kijijini hapo
kwa ajili ya mboga na kuwatumia
kwa kitoweo walianza kuugua hali
iliyosababisha kukimbizwa katika
Kituo cha Afya cha Msata ambako
walilazwa ya matibabu. Mama huyo
ambaye ni mkazi wa kijiji hicho,
lakini bado hajajulikana jina lake
anatafutwa ili aweze kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria kujibu
tuhuma hizo zinazomkabili, alisema
Bw Mangu.
Alisema kuwa watu 33 walitibiwa
na kuruhusiwa huku watu saba
wakiwa bado wamelazwa kutokana
na hali zao kuendelea kuwa mbaya.
Aliwataja watu ambao bado
wamelazwa wakiendelea kupata
matibabu katika Kituo hicho cha
Afya cha Msata kuwa ni pamoja
na mtoto Aksam Fadh( 3) Mkazi
wa Msata, Zaituni Katani (12)
mtoto Leila Mbaraka ( 2), Huruma
Othman, (16) Bi. Jamilah Hussein
(25) Bi. Shamila Ramadhani, Bw.
na Kesi Said.
Aliongeza kuwa, uchunguzi
unaendelea ili kuhakikisha kuwa
mama huyo anapatikana kwa
hatua zaidi za kisheria kufuatia
hali hiyo wakazi mkoani Pwani
wametahadharishwa kutokula
vyakula wasivyokuwa na uhakika
navyo ili kuepukana na matatizo
kama hayo.
No comments:
Post a Comment