30 March 2012

Serikali yabebeshwa lawama Kondoa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MA D I WA N I w a Ha lma s h a u r i y a Ko n d o a mk o a n i Dodoma wamesema kuwa wanakerwa na kitendo cha wagonjwa kuchangishwa fedha za kununulia mafuta ya gari la kubebea wagonjwa pindi wanapotakiwa kupelekwa katika vituo vya afya au hospitali.

Madiwani hao walitoa kauli
hiyo jana wakati wa kikao cha
kawaida cha Baraza la Madiwani
kilichofanyikia katika Halmashauri
ya Kondoa.
Walisema, kitendo cha Serikali
kutokutoa fedha za kutosha katika
halmashauri hususan idara ya afya
hali hiyo imechangia wagonjwa
kuchangishwa fedha za kununulia
mafuta pindi wanapotakiwa kutumia
gari la kubebea wagonjwa.
Walidai kuwa kwa sasa wagonjwa
ambao wanatakiwa kubebwa na
magari ya halmashauri kwa ajili
ya kuwapeleka katika hospitali
kubwa kwa ajili ya kupata matibabu
zaidi huchangishwa fedha kwa ajili
ya ununuzi wa mafuta ya gari la
kubebea wagonjwa.
Wakichangia kuhusu kero hiyo
madiwani hao walisema, kutokana
na wagonjwa ama ndugu wa
wagonjwa kuchangishwa fedha
hizo inafikia hatua ndugu hao ama
wagonjwa wenyewe kushindwa
kuchangia mafuta na kukosa
matibabu kutokana na usafiri kuwa
mgumu.
"Nilazima Serikali itambue kuwa
sekta ya afya ni muhimu, hivyo
kuna kila sababu ya halmashauri
kupewa fedha za kutosha kwa
ajili ya kununulia mafuta ya
kutosha kwa ajili ya magari ya
kubebea wagonjwa. Kwa sasa
uchumi ni mbaya unapomwambia
mgonjwa achangie mafuta kwa
ajili ya ununuzi wa mafuta ya gari
ya kubebea wagonjwa kamwe
hakuelewi, anakuona kama
mbabaishaji ama viongozi wa
halmashauri wanatafuna fedha,"
alisema mmoja wa madiwani hao
wakati akichangia.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya
Kondoa, Isdor Mwalongo alisema,
ni kweli kuwa wapo baadhi ya
wagonjwa ama ndugu za wagonjwa
ambao wanachangishwa fedha za
kununulia mafuta ya gari la kubebea
wagonjwa.
Alisema, tatizo hilo linatokana
na ukata na ufinyu wa bajeti ya
Serikali lakini hata hivyo serikali
inapambana ili kumaliza tatizo hilo
na kuwafanya wananchi kuachana
na kero hiyo.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo
alisema wagonjwa hawapaswi
kuchangia fedha kwa mtindo wa
kununua mafuta ya gari la wagonjwa
bali inafanyika hivyo kutokana na
halmashauri kutokuwa na fedha za
kuendeshea shughuli mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Kondoa, Bw. Khamisi Mwenda
aliwataka madiwani kuwa
wavumilivu juu ya tatizo hilo kwani
kwa sasa Serikali ina ukata mkubwa
wa kifedha na tatizo hilo linatokana
na mtikisiko wa uchumi duniani.
Bw. Mwenda alisema, Tanzania
p amo j a n a n c h i n y i n g i n e
zinakabiliwa na kuanguka kwa
uchumi hivyo hakuna mtu ambaye
anafurahishwa na kitendo cha
kuwachangisha wagonjwa kwa
ajili ya kununua mafuta ya gari la
kuwabebea wagonjwa.

No comments:

Post a Comment