Na Agnes Mwaijega
BARAZA la jipya la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limetakiwa kuwa makini na kuafanya mabadiliko makubwa kwa kuhakikisha linasajili wauguzi na wakunga wenye sifa zinazostahili ili kuboresha huduma za afya.
Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda alitoa mwito huo Dar es Salaam jana kwenye hafla ya uzinduzi wa baraza hilo.
Alisema utafiti unaonesha kwamba wauguzi hawazingatii maadili ya kazi yao ,sheria na miongozo. Alisema wauguzi wanatumia kauli mbaya na lugha isiyofaa kwa wagonjwa.
"Niseme ukweli kwamba baadhi ya malalamiko yanayoripotiwa na wagonjwa kuhusu watendaji wa afya ni ya kweli, hivyo yanatakiwa kutokomezwa kwa njia ya kuboresha utoaji wa huduma na nyie mkiwa wasimamizi wakuu wa utekelezaji," alisema
Alisema hali hiyo imewajengea taswira mbaya kwa wagonjwa na kusababisha huduma za afya kushuka.
"Naomba baraza lihakikishe kwamba wauguzi wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na kiapo cha taaluma yao ili waweze kuwa na taswira nzuri kwa jamii.
Dkt.Mponda alisistiza kuwa baraza linawajibika kuhakikisha wauuguzi ambao ndiyo watoa huduma wakubwa katika sekta ya afya wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu na ufanisi.
Aliwataka viongozi wa TNMC kuongoza baraza hilo kwa kuzingatia taratibu na kanuni ili kuiletea heshima taaluma ya ukunga na uuguzi nchini.
No comments:
Post a Comment