Na Pamela Mollel, Arusha
KATIBU wa Itikadi na Uenezi Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape
Nnauye ametua Jimbo la Arumeru
Mashariki tayari kwa kumnadi mgombea
ubunge wa jimbo hilo, Bw. Sioi Sumari na
ametamba kutetea ushindi wa chama chake
huku akidai Bw. Joshua Nasari wa CHADEMA
ni msindikizaji katika kichanganyiro hicho.
Bw. Nnauye alisema, mgombea
wa CHADEMA, Bw. Joshua Nassari ni
msindikizaji kwa kuwa ana uhakika Aprili
Mosi CCM kitaibuka kidedea hivyo sasa yuko
kwa ajili ya chama chake.
Aliyasema hayo jana wakati akimnadi
mgombea wa chama chake katika eneo la
Makumira wilayani Arumeru ambapo umati
mkubwa wa watu wakiwepo wanafunzi wa
Chuo Kikuu Makumira walishiriki.
Alisema, wanaopita na kusema 'patachimbika
na damu itamwagika' hawana uchungu na
Wana Arumeru hivyo wawapuuzie kwa
kuwa wanaubinafsi hivyo ni bora viongozi
CHADEMA wajihudhulu kwa kuwa
wameshindwa kazi katika kinyanganyiro cha
ubunge
Nawashaanga...sana eti wanasema kuwa
damu itamwagika hapa Arumeru hizo ni dalili
za Chadema kushindwa katika uchaguzi huu,
alisema Bw.Nnauye.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba mgombea
wa Chadema, Bw. Nassari yuko katika
kinyanganyiro hicho kwa lengo la kumsindikiza
mgombea wa chama chake, Bw. Sumari kwa
kuwa ndiye mshindi wa kiti cha ubunge katika
jimbo hilo.
Alisema, mara baada ya pingamizi la
Chadema lilipotupwa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Nassari
alichanganyikiwa kwa kuwa alitambua ya
kwamba, Bw. Sumari atakuwa mbunge wa
jimbo hilo bila kipingamizi.
Pia aliwaambia wakazi wa Makumira
kwamba ametua wilayani humo ili
kuwakumbusha wakazi wa wilaya hiyo
kwamba mshindi wa jimbo hilo ni, Bw.
Sioi Sumari na mgombea wa Chadema ni
msindikizaji katika uchaguzi huo.
Naye mgombea Ubunge, Bw. Sioi Sumari
alisema endapo watamchagua awe mwakilishi
wa jimbo hilo atahakikisha mikopo kwa
wanafunzi wa Chuo cha Makumira anasimamia
kwa ukaribu ili waweze kupata mikopo hiyo
kwenye halmashauri zao.
Alisema, Serikali iliyopo madarakani ni
ya CCM hivyo ataweza kutatua matatizo
mbalimbali yanayowakabili wanachuo hao
pamoja na wananchi wa eneo hilo.
Nape ni nani? hana sumu si lolote, wala hana hoja!!
ReplyDeleteNape anachotaka kuwahakishia ni kwamba Tume ya Uchaguzi imeshamaliza kazi ya kuchakachua kura ili kuipa ushindi CCM.Kwa hiyo hajivuni hivi hivi,maana ukweli ulipo CCM haikubaliki Arumeru licha ya kutumia uongo na matusi kuwasema wapinzani.
ReplyDelete