22 March 2012

Wassira azidi kumbana Slaa

  • Adai ana ushahidi wa fedha alizokula ujio wa  Papa II
  • Amtaka asitupie kanisa mzingo, ajitokeze kujibu mapigo
 Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakinyoosha mikono kuahidi  kukipigia chama hicho kura katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 mbele ya Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba (yahupo pichani) alipohutubia katika viwanja vya Mwembeyanga, Tandika Dar es Salaam jana (Picha na Peter Mwenda)


Na Peter Mwenda
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba  amesema inawezekana kabisa kwa kila mtanzania kulipwa sh. 450,000 kwa mwaka zinazotokana na rasilimali za asili.

Akizungumza na wanachama na wafuasi wa chama hicho kwenye viwanja vya Mwembeyanga Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema watanzania watalipwa fedha hizo kama watakiingiza kwenye katiba mpya kipengele hicho.

"Tanzania kuna rasilimali za asili nyingi, bahari, gesi, madini ya dhahabu, tanzanite, mbuga za wanyama na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuingia sh. bil. 2 kwa mwaka ambazo zinatosha watanzania kukagawana sh. 450,000 kwa mwaka" alisema.

Alisema wafuasi wa CUF wasitishike na helkopta zinazoranda kwenye chaguzi kuwa vyama hivyo havina uwezo wa kuleta mabadiliko kwa watanzania ambao wamekata tamaa kutokana na kukosa ajira.

"CCM na vyama vingine vinavyoongozwa na wapiga disko haviwezi kuwakombioa watanzania akimaanisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho Mwenyekiti wake anamiliki ukumbi wa Billicanas.

Alisema uchumi wa Tanzania unazidi kuwa taabani kwa sababu gharama za kuyingia tani 100 kutoka China ni nafuu kuliko kusafirisha tani moja kupeleka mkoa wa Kigoma na kuongeza kuwa rasilimali ambazo Tanzania inazo zinakosa viongozi wa kuzisimamia na badala yake zibnaingia kwenye mikono ya mafisadi.

Profesa Lipumba hata hivyo alimsifu Rais Jakaya Kikwete kukubali kuruhusu uundaji mchakato wa kuanzisha Katiba Mpya na kuongeza kuwa napaswa kuungwa mkono.

Alisema ili mipango hiyo itimie watanzania wote wakubali kujiandikisha kupewa vitambulisho na kuchangia kuundwa kwa Katiba mpya ambayo itasema kila mtanzania alipwe rasilimali za nchi.

Awali Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema wanaopiga kelele kuwa CUF imekufa wanajidanganya kwa sababu mapokezi wa Profesa Lipumba Machi 11 mwaka huu ni ushahidi tosha kuwa chama hicho hakitakufa kamwe.

"Mimi nilitoa machozi baada ya kuona umati mkubwa ulijitokeza kumpokea Mwenyekiti wetu, hiyo ni salamu kwamba tumeanza mikakati ya kuingia Ikulu, tumeingia mguu mmoja Zanzibar, mwaka 2015 tunaingia miguu yote je, Ikulu ya magogoni mnasemaje?aliuliza Maalim Seif na kuitikiwa na sauti kuwa CUF inachukua dola.

Katika mkutano huo CUF imetoa namba 15338 kwa njia ya mtandao wa zantel ambayo mwanachama wake atachangia kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa 2015 ambako pia aliywahi kuwa kiongozi wa chama hicho na baadaye kuhamia CCM, Bw. Hamisi Kituga amerejea katika chama hicho na kukabidhiwa kadi na Mwenyekiti Profesa Lipumba.

Pia Mjumbe wa baraza Kuu la Taifa la chama hicho kutoka mkoa wa Mbeya, Bw. Yassin Mrotwa ambaye alikuwa mmoja wa wanachama walioshtaki mahakamani amejitoa na kurudi CUF.

13 comments:

  1. Profesa nakuamini. Hilo la kupata mgao lawezekena tena siyo 450,000/= kwa mwaka bali kwa mwezi kama mafisadi na wala rushwa watadhibitiwa.
    Tanzania tuna National park 15 game reserves & Game parks zaidi ya 40. Hakuna mkoa usiokua na madini. Kwakuitaja baadhi.
    Kilimanjaro , Road light, Rubby, ARUSHA = Tanzanine,Hamasist,Roadlight,Mecury, Kanda ya ziwa. Dhahabu & Almasi. Mikoa ya kusini = Green Garnet nk.

    Hebu tulinganishe hivyo nilivyotaja na nchi kama BOTSWANA ambayo wanategemea Almasi na mifugo na ni nchi yenye uchumi mzuri tu.
    Kigezo cha idadi ya watu siyo tija.

    ReplyDelete
  2. Uprofesa wa Lipumba unatia mashaka endapo anataka wote tuwe wanasiasa. Kupiga disko ni kazi halali hivyo asitukashifu sie wanamuziki na wapiga disco. Yeye atoe sera zake. Ina maana anataka wote tuombe ajira serikalini? Hata yeye akiingia Magogoni atatoa ajira kwetu sie wanamuziki? Kama yeye hana mapenzi na muziki/disco basi atuachie starehe zetu yeye akalale. Hizo zake ni mufilisi!

    ReplyDelete
  3. Mkutano huu umekosa bahati, Tangia ulipofanyika siku ya Jumatano, huko Muembe yanga, inashangaza kwamba habari zake hazijaandikwa popote, si redioni wela magazetini(isipokua hili la Majira).
    Labda kunamgomo baridi, au tunasubiri Hamad Rashid ahutubieee!!!!!

    ReplyDelete
  4. Wana habari Au wamiliki wa vyombo vya habari anzania acheni ushabiki wa CCM na Chadema,vyama hivi viwili vinachosha kusoma habair zao kwenye magazeti yenu,au mmekatazwa kuandika habari za vyama vyengine achane ubaguzi wenu wa wazi wazi Mikutano ya hao Cuf hatujaiona kuandikwa kwenye magazeti yenu mna maana gani au Serikali imewazuia,punguzeni ushabiki wa CCm na Chadema na hivyo vyama vyengine andikeni habari zake pia.

    ReplyDelete
  5. Kama ingekuwa mkutano huo kahutubia Hamad Rashid na kuinanga CUF coverage yake ingekuwa kubwa sana.

    ReplyDelete
  6. Lipumba anatakiwa aelewe kuwa miongoni mwa hao anaowahutubia, wapo wengi tu waliopata ahueni ya maisha kupitia muziki. Wapo vijana wengi tu wanaoimba bongo fleva, taarab na nyimbo nyingine. Sasa kama anakashifu wapiga miziki, simuelewi kabisa wakati hata yeye anajua vijana wakikosa ajira athari zake ni mbaya. Nitampinga kwa hili la kuuona muziki ni uhuni, hayo mawazo ya zamani hata walugaluga wengine walishaacha kuyaamini, sasa iweje profesa wa uchumi aone muziki ni uhuni? Anatukatisha tamaa wengine tunaojaribu kutoka kupitia muziki

    ReplyDelete
  7. LIPUMBA USIDHARAU MUZIKI KWANI NI AJIRA YA VIJANA WENGI TU

    ReplyDelete
  8. CUF MNATUDANGANYA MNGEKUWA MNATAKA KUTUOKOA WATANZANIA MBONA MMEFUNGA NDOA NA CCM ZANZIBAR.TUMEWAGUNDUA MNATUDANGANYA.IPO SIKU NAYE LIPUMBA ATAPEWA UMAKAMU NA CCM AKAKUBALI .MNAWADANGANYA WATU WANAOONA KWA MACHO YOTEEEEE.MMESHITUKIWA CUF

    ReplyDelete
  9. CUF MNATUDANGANYA MNGEKUWA MNATAKA KUTUOKOA WATANZANIA MBONA MMEFUNGA NDOA NA CCM ZANZIBAR.TUMEWAGUNDUA MNATUDANGANYA.IPO SIKU NAYE LIPUMBA ATAPEWA UMAKAMU NA CCM AKAKUBALI .MNAWADANGANYA WATU WANAOONA KWA MACHO YOTEEEEE.MMESHITUKIWA CUF

    ReplyDelete
  10. cuf ni mdigo wake na ccm hivyo lipumba anatudanganya watu na akili zetu.naye ni kama maalim seif alivyouza chama huko ,zanzibar hivy CUF NA CCM LAO NI MOJA .WATANZANIA MUDA WA KUDANGANYWA UMEPITA HUU NI WKT WA KUJITAMBUA

    ReplyDelete
  11. Kuhusu Wassira ningekuwa kwenye mkutano wake huku Arumeru ningemuuliza kwa nini huwa analala wakati akiwa bungeni.... tehe tehe.

    ReplyDelete
  12. Mheshimiwa Mzee wetu Waziri Wassira.
    Usijidhalilishe mbele ya Watanzania wote. Ukiwa Arumeru ni kama uko na Watanzania wote kimtandao.

    Kama uko ushahidi wa kuliwa fedha za Ujio wa PAPA umeambiwa nenda mahakamani. Kama huendi, kauchukue ushahidi huo na uuchapishe magazetini au kwenye TV au Radio. Kama sivyo hatutakosea tukikuita Mzee KIJANA MSANII na mmbea.

    Usimwogope SLAA. Mkomeshe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hawa wote wezi wanatumia ushabiki wa kisiasa kuficha madhambi yao. watanzania mnaliwa na wanasiasa huku mkijazana kwenye mikutano yao mzidi kuliwa. amkeni waambieni waache siasa za ghiliba. mbunge atapata wapi pesa za kukuondolea kero? amka zinduka mtanzania. helikopta zinazoruka angani ni pesa yenu inachomwa na malawansi kibao wanapeana huko

      Delete