30 March 2012

Wananchi wasiohudhuria mikutano waadhibitiwe

Katiba ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania inafafanua kuwa
Serikali za mitaa, Vitongoji, Vijiji
ni vyombo muhimu vya wananchi
katika ngazi ya msingi ya serikali
ambazo huundwa, huendeshwa,
husimamiwa na kuwajibika kwa
wananchi wenyewe.

Hivyo zimeundwa kuwawezesha
wananchi kushiriki katika masuala
ya siasa, uchumi, upatikanaji wa
huduma na utawala katika maeneo
yao na katika nchi yao.
N i m u u n d o a m b a o
unawawezesha wananchi kuwa
na udhibiti wa maamuzi ya
wawakilishi waliowachagua
ambapo kwa mtazamo huu wa
kikatiba, serikali za mitaani,
vitongoji au vijiji ni fursa kwa
wanajamii kukuza demokrasia na
ushiriki wao katika maendeleo ya
maeneo yao.
Ni vyema ieleweke kuwa,
serikali za mitaa si wakala wa
serikali kuu bali ni serikali kamili
zenye mamlaka chini ya sheria
kama ilivyoelezwa katika Katiba.
Kwa kutambua umuhimu huo
Mtandao wa Asasi za Kiraia
Mkoa wa Tanga (TASCO)
unafanya kazi ya kuwajengea
uwezo wananchi wa majimbo ya
Mkoa huuo kutambua wajibu wa
serikali hizo katika kuwawezesha
kutambua nafasi yao kushirikiana
kupanga mipango ya maendeleo
na viongozi wao wa kuchaguliwa.
Katika mdahalo uliofanyika
Maramba wilaya ya Mkinga
ulioratibiwa na TASCO kwa
ufadhili wa The Foundation For
Civil Society wananchi wengi
walionesha wasiwasi wao juu
ya mamlaka yaliyowekwa kwa
wananchi kuwaondoa viongozi
wao wa vijiji ambao hawaitishi
mikutano ya vijiji huku kukiwa
hakuna kipengele kinachoonesha
wananchi watawajibika vipi pindi
watakaposhindwa kuhudhuria
mikutano hiyo muhimu kwa
maendeleo.
Katika Mada zilizowasiliwa
na Mtaalamu aliyeboboea katika
masuala ya Sheria na Katiba
ambaye pia ni Hakimu Mkazi
wa Mahakama ya wilaya ya
Handeni,Bw Mgongolo Jonathan
aliweza kuanisha majukumu ya
wananchi katika Serikali hizo za
Vijiji kisheria.
M i o n g o n i mw a
majukumu hayo ni ya
kisheria na kiutawala
wananchi wanatarajiwa
kutekeleza majukumu
kama kuelewa Sheria zote
zinazohusu serikali za
Mitaa na kuishi kufuatana
na sheria hizo.
Pia, kutambua nafasi ya
mwananchi katika jamii na
kushiriki katika shughuli
mbalimbali za maendeleo, kudai
haki zake za msingi kutoka kwa
viongozi wake, kuhakikisha kuwa
viongozi wanatimiza wajibu wao
kama ipasavyo.
Kadhalika kama viongozi
hakutimiza wajibu wake, ni
jukumu la wananchi kumwondoa
madarakani kwa kufuata sheria
kama vile kumpigia kura ya
hapana. katika Kifungu cha14
(4) cha sheria a serikali za mitaa
(Mamlaka ya miji) Na.8 ya mwaka
1982 ambacho kinaweza kutumika
kutekelezwa matakwa hayo.
Pamoja na majukumu ya
wananchi kuyaainisha muhimu
pia kutambua majukumu ya
mkutano mkuu wa vitongoji
ambapo kisheria ni pamoja na,
kupokea na kujadili taarifa za
utekeleaji wa shughuli mbalimbali
za kitongoji zitakazowasilishwa na
Mwenyekiti wa kitongoji.
Mengine ni kujadili hali ya ulinzi
na usalama na maendeleo katika
eneo la kitongoji, kuweka mikakati
ya kupambana na ugonjwa wa
UKIMWI, kupokea maelekezo
kutoka kwa Halmashauri ya kijiji
na kuweka mikakati ya utekelezaji
wake katika kitongoji.
Kwa maana hiyo basi, mkutano
mkuu wa kitongoji ni muhimu sana
katika utekelezaji wa mipango
ya maendeleo ya kijiji pale
ambapo mikutano hiyo inafanywa
kuna mafanikio makubwa ya
maendeleo.
Pia ni muhimu kutambua wajibu
na majukumu ya mkutano mkuu
wa mtaa ambayo ni kupokea na
kujadili taarifa kuhusu miradi
inayoendeshwa katika eneo la
mtaa na maendeleo yake, hali ya
ulinzi na usalama.
Mengine ni maamuzi ya Kamati
ya maendeleo ya kata au ya
Halmashauri ya mji,manispaa au
jiji kupitia kamati ya maendeleo ya
Kata yanayohusu mtaa,Maamuzi
ya kamati na utekelezaji wake.
Nimetumia muda mwingi
kueleza mfumo na wajibu wa
serikali kwa wananchi sasa
nageuza kibao kwa wananchi
kuendesha midahalo ngazi ya
Vijiji kuliko ilivyo sasa kufanyika
ngazi ya majimbo pekee ili kutoa
mwanya mpana zaidi kwa watu
kujitambua ili waweze kuwa na
mchango katika kuleta maendeleo.
0776-989851

No comments:

Post a Comment