Bw. Lyanga aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa kuwa ni Bw. Saidi Kaluguli (49) mkulima mkazi wa kijiji cha Ishololo,
Bw. Daudi Lazaro (30) mkazi wa kijiji cha Igalamya, Bw. Lucas Sengo (40) mkazi wa kijiji cha Usule na Bi. Agnes Leo (33) mkazi
wa Igalamya.
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga
linawashikilia watu saba akiwemo
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Igalamya wilayani Shinyanga na ofisa
mtendaji wake wakituhumiwa kwa kosa la
wizi wa chakula cha msaada kilichotolewa na
serikali.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Shinyanga, Bw. Onesmo Lyanga aliwataja
viongozi wa serikali ya kijiji waliokamatwa
kuwa ni, Bw. Maige Nkengi (58) ambaye ni
mwenyekiti wa serikali ya kijiji na ofisa mtendaji
wake wa kijiji, Bw. Mabana Luhende (37) wote
wakazi wa kijiji hicho cha Igalamya.
Bw. Lyanga alisema mbali ya watuhumiwa
hao ambao walikamatwa Machi 25, mwaka
huu saa 1.00 asubuhi kijijini humo pia polisi
walimkamata Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata
ya Usule wilayani Shinyanga aliyetajwa kwa
jina la Bw. Kabika Jumanne (57).
Alisema, viongozi hao watatu pamoja na
wanakijiji wengine wanne wote kwa pamoja
wanatuhumiwa kula njama na kuiba magunia
31 ya mahindi yenye thamani ya sh. 930,000
yaliyolewa na Serikali kama msaada kwa ajili ya
wakazi wa Kijiji cha Igalamya wanaokabiliwa
na njaa.
Bw. Lyanga aliwataja watuhumiwa wengine
waliokamatwa kuwa ni Bw. Saidi Kaluguli
(49) mkulima mkazi wa kijiji cha Ishololo, Bw.
Daudi Lazaro (30) mkazi wa kijiji cha Igalamya,
Bw. Lucas Sengo (40) mkazi wa kijiji cha Usule
na Bi. Agnes Leo (33) mkazi wa Igalamya.
Bw. Lyanga alisema, baada ya kupatikana
kwa taarifa juu ya upotevu wa mahindi hayo
ya msaada polisi kwa ushirikiano wa raia wema
waliendesha msako mkali ambapo walinzi
wa jadi sungusungu walifanikiwa kukamata
magunia 20 na mengine 11 yalikamatwa na
polisi kwa msaada wa wananchi.
Alisema, mara baada ya kukamatwa kwa
mahindi hayo ndipo taratibu za kuwakamata
watuhumiwa wote zilipofanyika na kwamba
baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa
mahakamani kujibu shtaka lao la wizi wa
chakula cha msaada.
No comments:
Post a Comment